Breaking News

CUF YALAANI MAUAJI YA MTOTO ASIMWE NOVATH

Jana Juni 18, 2024 CUF-Chama Cha Wananchi tulitoa TAMKO kufuatia Kuuawa Kinyama kwa mtoto Asimwe Novath huko Biharamulo, Kagera. Pamoja na kutoa Salamu za Pole na RAMBIRAMBI, tulitoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha watuhumiwa wa mauaji haya yanayochagizwa na Imani za Kishirikina wanakamatwa mara moja na kufikishwa Mahakamani.

CUF- Chama Cha Wananchi kinalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hii iliyofikiwa.