Breaking News

BRELA WANANCHI SAJILINI MAJINA YA BIASHARA ZENU

Mkuu wa Sehemu ya Makampuni, kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Lameck Nyange akiwasilisha mada juu ya elimu ya Sheria ya Majina ya Biashara kwa waandishi wa habari wanaoripoti kutoka Mkoa wa Dar es Salaam. Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 19 Juni, 2024 mkoani Morogoro.

Morogoro
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa wito kwa Wananchi kuwa na mwamko wa kusajili majina ya biashara zao.

Wito huo umetolewa mapema leo Juni 19, 2024 na  Mkuu wa Sehemu ya Kampuni kutoka Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara wa BRELA, bwana Lameck Nyange wakati akiwasilisha mada katika siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari wanaoripoti habari za biashara kutoka mkoani Dar es Salaam kuhusu Majina ya Biashara (Sheria na huduma baada ya Sajili) yanayofanyika mkoani morogoro.

Alisema moja ya faida ya kufanya usajili wa majina ya biashara ni pamoja na kusaidia kumlinda mwanzilishi wa jina hilo ili lisijekuchukuliwa na kusajiliwa na mtu mwingine jambo litakalopelekea yeye kupoteza umiliki wake.

"Nitoe rai kwa wananchi kusajili majina ya biashara ni muhimu sana kwa ajili ya kumlinda mmiliki wa jina husika. Hii itasaidia kuzuia BRELA na kumtambua na kuzuia kulisajili kwa mtu mweingine. Kila mfanyabiashara ni muhimu kusajili majina ya biashara zao," Alisema Bw. Samson.

Alisema faida nyingine ya kusajili jina la biashara, ni pamoja na kuwasaidia BRELA kutoruhusu kulisajiliwa tena jina hilo na mtu mwingine

Aidha bwana Samson aliongeza na kubainisha kuwa majina ambayo hayawezi kusajiliwa ni pamoja na majina ambayo kwa namna moja ama nyingine ni matusi, majina ambayo yanataja jina ama chombo cha Serikali.

"Wakati wa usajili wa majina ya biashara kunabaadhi ya majina ayawezi kusajili kutokana na vigezo vilivyoweka mfano jina ambalo lina maana ya matusi ua kutaja chombo chochote cha serikali" Alisema Bw. Samson.

No comments