Breaking News

UPDATE: MWENENDO WA KIMBUNGA "HIDAYA" KATIKA BAHARI YA HINDI MASHARIKI MWA PWANI YA TANZAΝΙΑ

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa Kimbunga 'HIDAYA' ambapo kinasafiri katika eneo la Bahari kikiwa na mgandamizo wa hewa wa kiasi cha 981hPa na kasi ya upepo unaofika kilomita 130 kwa saa

TMA imesema matarajio ni kwamba kimbunga “Hidaya” kitaendelea kusogea karibu kabisa na ukanda wa Pwani ya Tanzania usiku wa leo Mei 3, 2024 na mchana wa Mei 4, 2024 na baadaye kitapungua nguvu Mei 5, 2024

Kimbunga HIDAYA kinatarajiwa kusababisha vipindi vya Mvua kubwa na upepo mkali katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam na maeneo ya Unguja

Ili kuepuka madhara, TMA imeshauri Watu kuchukua tahadhari hasa wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Ukanda wa Bahari ya Hind