WIKI YA AZAKI 2023 KUZILETA PAMOJA ASASI ZA KIRAIA 500 KUJADILIANA JUU YA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KWA MATOKEO CHANYA JIJINI ARUSHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akifafanua jambo katikamkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maandalizi ya mkutano wa Wiki Ya Azaki 2023 makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Bi Nuria Mshale kutoka Malala Fund akizungumza katika mkutano na waandshi wa habari (hawapo pichani) juu ya mada zitakazo wasilishwa katika mkutano wa Wiki Ya Azaki 2023 itakayofanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 27 jijini Arusha.
Dar es salaam:
Washiriki zaidi ya 500 kutoka Asasi za kiraia, Serikalini na wadau wa maendeleo wanatarajiwa kushiriki katika wiki ya AZAKI 2023 ambayo inataraji kuanza Oktoba 23 hadi 27 jijini Arusha.
Akizungumza mapema leo oktoba 17, 2023 jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Bwana Francis Kiwanga amesema kongamano la mwaka huu litakuwa la kipekee kwani washiriki watapata fursa mbalimbali ikiwemo ya kukutana na wadau wa maendeleo.
“Wiki ya AZAKI 2023 itakuwa na fursa kubwa kwa washiriki kutoka katika Sekta ya AZAKI ikiwa na kuwaleta pamoja na kuchangamana na wadau wa Maendeleo,” Alisema Bw. Kiwanga
Alisema washiriki wa Wiki ya AZAKI 2023 pia watapata wasaa wa kujadili masuala ya yanayohusu Maendeleo ya Taifa na wadau mbalimbali kutoka Asasi za kiraia, Serikali, wananchi, wanazuoni na Sekta Binafsi.
Alisema kupitia kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni teknolojia na jamii. washiriki watapata wasaa wa kujadiliana na kiangalia walipotoka, walipo sasa na wanakokwenda pamoja na kubadilishana mawazo, uzoefu na maarifa juu ya matumizi ya teknolojia kwa matokeo chanya ya kijamii nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Malala Fund, Bi Nuria Mshale amesema Katika Wiki Ya Azaki 2023 washiriki watapta wasaa pia wa kutajadili mchango wa teknolojia katika kuboresha elimu, majukwaa ya kujifunza kupitia mtandao, na mafunzo ya walimu ili kuboresha matokeo ya ujifunzaji na kuziba mapengo ya kielimu.
"Katika wiki ya Azaki 2023 washiriki watapta wasaa pia wa kutajadili mchango wa teknolojia katika kuboresha elimu, majukwaa ya kujifunza kupitia mtandao, na mafunzo ya walimu ili kuboresha matokeo ya ujifunzaji na kuziba mapengo ya kielimu" Alisema Bi. Mshale.
Alisema Katika Wiki Ya Azaki 2023 mada tofauti zitawasilishwa ikiwemo zitakazojikita katika kutathmini kauli mbiu ya teknologia na Jamii, Ikiwemo; Ujumuishi na Uwezeshaji wa Kidijitali na kutafakari kuhusu ujumuishi wa watu wenye ulemavu na matumizi ya teknolojia”
Wiki ya Azaki 2023 imebeba Kauli mbiu ya mwaka yenye lengo la kuzileta pamoja Asasi za Kiraia, watunga sera, wanateknolojia, na wadau kubadilishana mawazo, uzoefu na maarifa juu ya matumizi ya teknolojia kwa matokeo chanya ya kijamii nchini Tanzania
No comments