BODI YA UTALII TANZANIA YAISHUKURU SERIKALI KWA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA SEKTA YA UTALII
Mkurugenzi wa Masoko TTB, Dokta Gladstone Mlay akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari juu ushindi Tuzo ya Bodi bora ya utalii Afrika katika mashindano ya World Travel Award 2023 jijini Dar es salaam.
Afisa Masoko kutoka kampuni ya ZARA TOURS, Bi. Nancy Ngotea akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa hatua inazozichukua mpaka kuiwezesha kuibuka mshindi wa bodi bora ya utalii Afrika katika mashindano ya World Travel Award 2023.
Akizungumzia jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Masoko TTB, Dokta Gladstone Mlay amesema kufuatia jitihada hizo uwekezaji mkubwa uliofanywa serikali katika sekta ya utalii Tanzania imekuwa ikindelea kufanya vizuri kimataifa.
“Rais Dkt Samia tangu aingie madarani amekuwa akichukua hatua za makusudi ambazo zimesaidia Tanzania kuendelea kushinda tuzo mbalimbali za kimataifa hususani tuzo ambayo imeshinda hifadhi ya Serengeti kwa kuwa mshindi wa kwanza kwa kipindi cha miaka mitano mfurulizo hifadhi bora za taifa" Alisema Bw. Mlay.
Amesema pia Tanzania mwaka tena imefanikiwa kushinda tuzo nyingine ambapo Ngorongoro imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kivutio bora Afrika
Aidha Bwana Mlay aliongeza kuwa pamoja na nchi kuendelea kushinda katika vipengele hivyo vya utaliii pia kwa Mara 7 mfurulizo kisiwa cha Thunder kilichopo Mafia ndio kimechukua namba moja Afrika kimeweza kushinda katika kipengere cha visiwa vyenye hadhi .
Bw. Mlay ametaja tuzo nyingine kuwa ni kipengele cha kampuni bora za utalii Tanzania ambapo katika lipemgere hocho kampuni ya ZARA TOURS ndio imeibuka mshindi.
Kwa upande wake Afisa Masoko kutoka kampuni ya ZARA TOURS, Bi. Nancy Ngotea ameishukuru serikali kwa hatua ambazo imekuwa ikizichukua ikiwemo kuweka mazingira mazuri kwenye sekta ya utalii kwani ndio imeleta ushindi huo kwa taifa.
"Mafanikio haya makubwa ambayo yanaendelea kupatikana katika sekta ya utalii yamechochewa na jitihada za Rais Dkt. Samia kupitia filamu ya the Royal Tour imeweza kuifungua nchi kimataifa" Alisema Bi. Ngotea.
No comments