TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA PILI WA KIMATAIFA WA KUTOKOMEZA UKEKETAJI
Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dokta Dorothy Gwajima akifafanua jambo juu ya maandalizi ya mkutano wa pili wa kimataifa wa kutokomeza ukeketaji ambao utawakutanisha pamoja washiriki zaidi ya 900 kutoka nchi mbalimbali barani afrika.
Mkurugenzi wa idara ya watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum bwana Sebastian Kitiku akizungumza ushriki wa tanzania katika mkutano huo wa pili wa kimataifa wa kutokomeza ukeketaji ambao utawakutanisha pamoja washiriki zaidi ya 900 kutoka nchi mbalimbali barani afrika.
Dar es Salaam:
Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa pili wa kimataifa wa kutokomeza ukeketaji ambao utawakutanisha pamoja washiriki zaidi ya 900 kutoka nchi mbalimbali barani afrika.
Akizungumza jijini dar es salaam juu ya maandalizi ya mkutano huo Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Dokta Dorothy Gwajima amesema mkutano huo utaanza oktoba 9 hadi 11 katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salam.
Alisema mkutano huo mwaka huu una kaulimbia isemayo "Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kizazi kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji (Change in a Generation) una lengo la kutoa fursa kwa wadau wanaopambana na ukueketaji kuunganisha nguvu pamoja kubadilishana uzoefu, kujengeana uelewa na maarifa katika kuimalisha mapambano dhidi ya vitendo vya ukeketaji katika bara la afrika.
Aidha dkt. Gwajima aliongeza kuwa pia mkutano huo unafanyika wakati maadhimisho ya siku ya kiamataifa ya mtoto wa kike ambayo ufanyika kila mwezi oktoba.
Alisema maadhimisho ya mwaka huu ni ya 12 tangu kuanza kuazimishwa na utekelezaji wa tamko la baraza kuu la umoja wa mataifa namba 66/180 la tarehe 19 decemba 2018. Lengo la siku hii ni kutamthimini jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na nchi wanachama wa umoja wa mataifa katika kuboresha upatikanaji haki, ulinzi, ustawi na maendeleo ya mtoto wa kike.
Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum bwana Sebastian Kitiku ameitaja baadhi ya mikoa ambayo takwimu zinaonyesha kuwa hali ya matukio ya ukeketaji ni manyara asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha asilimia 41.
Ameitaja mikoa mingine kuwa ni Mara asilimia 32, Singida 31, Tanga 14 ambapo serikali imekuwa ikichukua hatua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa elimu kwa jamii ili vitendo hivyo vitokomee nchini.
Tanzania imepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa kwanza wa kimataifa wa kutokomeza ukeketaji nchini Burkina Faso mwaka 2018 ambao jumla ya washiriki kutoka nchi 22 wanachama wa umoja wa afrika walishiriki.
Katika mkutano huo ambao uliadhimia kuwa kila kanda katika afrika ianzishe ushikiano wa kupambana na mila na desturi kupinga ukeketaji sambamba na kudhibiti mipaka hili kuzuia miingiliano wa mila hiyo kutoka nchi moja kwenda nyingine (Grossboader FCM) pamoja na kuandaa mikutano itakayofanyika kila baada ya kipindi fulami kwa kuoendekeza nchi itakayoteuliwa na kamisheni ya umoja wa afrika.
No comments