WADAU WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAZI WA UWEKEZAJI WA MIUNDOMBINU YA HALI YA HEWA NCHINI.
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Hali ya Hewa ya Denmark (DMI) kama Mshauri na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kama Taasisi ya kusimamia Utekelezaji wa mfuko (Programu) wa kuimarisha miundombinu ya hali ya hewa na ufanisi duniani kwa nchi zinazoendelea (Systematic Observations Financing facility-SOFF) imeandaa warsha ya wadau kujadali mpango kazi wa uwekezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya hali ya hewa nchini, tarehe 21 Septemba, 2023, Dodoma, Tanzania.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chang'a na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), alisema wataalamu kutoka TMA na DMI kwa ushirikiano wa pamoja wameandaa rasimu ya mpango kazi kwa kuzingatia mahitaji ya nchi na kuwakutanisha wadau ili kupata maoni ambayo yatasaidia kuboresha mpango kazi huo.
Aidha, Dk.Chang’a aligusia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SOFF nchini, mfuko ambao umekuwa ukichangiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na UNDP.
“Utekelezaji wa mradi huu nchini upo katika awamu tatu ambapo moja ya hatua za awali ni kutambua na kuainisha mahitaji ya nchi katika upande wa miundombinu ya hali ya hewa na kuandaa mpango kazi wa kushughulikia mahitaji yaliyo ainishwa ili koungeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma za hali ya hewa hususani kipindi hiki ambacho tunakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi”. Alisema Dkt. Chang’a.
“Hii ni mojawapo ya hatua muhimu ambayo inaenda kuchangia katika jitihada kubwa zinazofanywa na serikali yetu ya kuimarisha huduma za hali ya hewa na kuongeza uwezo wetu wa kuhimili changamoto za mabadiliko hayo ya hali ya hewa. Tunaishukuru sana Serikali na wadau wengine wa maendeleo”. Aliongezea Dkt. Chang’a.
Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka DMI, Bw.Christian Rodrup alisema anatarajia kupokea michango muhimu kutoka kwa wadau kwa ajili ya kuboresha rasimu ya mpango kazi, pia alisisitiza kuwa kati ya nguzo nne muhimu za utoaji
No comments