SHINDANO LA INSTAQUEEN LAZINDULIWA RASMI, KUFANYIKA DEC 5
Dar es salaam:
Mabinti wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shindano la kumsaka Instaqueen litaklofanyika Disemba 5 mwaka huu.
Akizungumza juu ya maandalizi ya shindano hilo jijini Dar es Salaam, Balozi wa Kampuni hiyo Meena Ally amesema mshindi wa kwanza wa shindano hilo ataibuka na zawadi ya milioni 3, wa pili milioni 2 wakati msindi wa Tatu milioni 1 pamoja na wote washindi wote kupata kazi ya kudumu.
“Instaqueen ni shindano la urembo la kidigitali ambalo washiriki wataonyesha uzuri, vipaji binafsi katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, haswa Instagram, ambapo washiriki watatuma picha na video zao fupi wakijielezea wasifu wao pamoja na ujumbe wa kuomba kujiunga na Instaqueen Tanzania,” Alisema Bi. Meena
Alisema shindano hili Mtu yeyote ambaye anakidhi vigezo na masharti ya Instaqueen anaruhusiwa kushiriki mashindano ya Instaqueen ni mwenye umri wa miaka 18-35, uraia wa Mtanzania picha zake ziwe za kimaadili.
"Instaqueen ilizaliwa kwa nia ya kutoa au kutengeneza jukwaa kwa watu kuonyesha uzuri na vipaji vyao pekee kidijitali, kwamba lengo lake ni kuwapa fursa watu walio wengi ambao wanatamani kutambulisha na jamii, kuwa watu maarufu na kuonyesha vipaji vyao" Alisema bi Meena
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa InstaQueen Tanzania, bwana Maximilian Donald amesema ili uweze kushiriki shindano la Instaqueen mshiriki hatatakiwa kutuma maombi, mchujo kupitia kura za wananchi ambayo ni hatua ya mtoano, kisha Nusu fainali na baadaye fainali yenyewe.
"Washiriki shindano la Instaqueen watapitia hatua mbalimbali kama kutuma maombi, mchujo kupitia kura za wananchi ambayo ni hatua ya mtoano, kisha Nusu fainali na baadaye fainali yenyewe" Alisema Bw. Donald.
Alisema shindano hilo la Instaqueen litatumia fursa na nguvu ya mitandao ya kijamii, kuweza vipaji vyao na kumpa mtu uhuru wa kushiriki shindano popote alipo na kuweza kupiga kura kwa mtu yeyote ampendaye.
Mapema akizungumza wakati akimkaribisha mkurugenzi, Dokta Kumbuka ambaye pia ni Balozi amesema shindano la Instaqueen limeanzishwa kwa lengo la kubadilisha mawazo ya Vijana hususani kutumia mitandao ya kijamii kwa maendeleo chanya kwao na kwa jamii inayomzunguka.
"Shindano hili itawasaidia washindani kujiamini, kuendeleza vipaji vyao katika tasnia ya urembo, kujifunza mengi kuhusiana na masuala ya urembo, na kupata kutambuliwa katika tasnia ya urembo na mitindo na cha pili Instaqueen inatoa fursa za Kazi na kuongeza ujuzi" Alisema Dkt. Kumbuka.
No comments