UTENDAJI WAIBEBA NIC INSURANCE KUPATA FAIDA
Dar es salaam:
Licha ya kugubikwa na milima na mabonde katika utendaji huku likikumbana na hatari ya kufutwa lakini bado NIC Insurance limesema mabadiliko ya kiutendaji ndani ya shirika hilo limefanya shirika hilo kupata faida.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa NIC insurance, Dokta Elirehema Doriye jijini dar es salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari ambapo amesema mikakati ya shirika hilo ndio siri ya kuendelea kwake kwani ndani ya kipindi cha miaka 55 tangu lianzishwe shirika hilo lilikuwa likipata hasara hali iliyosababisha kutoonekana tija ya uwepo wake.
Amesema hali mbaya ya shirika hilo nyuma ya mwaka 2019 ilitokana na uwepo watu wengi waliokuwa wanadai, ingawa baada ya uchambuzi baadhi ya watu walikuwa hewa,
Aidha Dr Doriye amesema Mabadiliko yaliyofanyika katika shirika hilo yaliakisi kwenye rasilimali watu na uwekezaji na kutoka kwenye mifumo ya kizamani na kwenda kwenye mifumo ya tehama, hali ambayo imechangia kupata faida
No comments