FAMILIA ZA WALIOHUKUMIWA KWA UGAIDI WAMWANGUKIA RAIS SAMIA,
Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania (Tauzakta) Kigozi Shabani Kigozi akifafanua jambo katika mkytano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tauzakta Mkoa wa Morogoro Sheikh Juma Kitungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam;
Wazazi na Walezi wa watoto waliohukumiwa kwa tuhuma za ugaidi wameomba kukutana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kumweleza ukweli wa jambo hilo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi ya Ukumbusho wa Zaka Tanzania (Tauzakta) iliyopo mkoani Morogoro Kigozi Shabani Kigozi akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wazazi hao.
“Tunaomba kukutana na Rais, tumweleze Ukweli kwani hawa watu hawajatandewa na wanadhulumiwa. Tunaomba mtufikishie kilio chetu kwa Rais kwamba aliowapa madaraka wamsaidie wamelewa madaraka na kuonea wananchi wasio na hatia,” ameeleza Kigozi.
Amesema kwamba waliohukumiwa ni watu 21 kwa vifungo vya miaka tofauti tofauti vya Kati ya miaka 10 hadi 30.
Kigozi amebainisha kwamba Kati ya hao watu tisa wamehukumiwa miaka 10, wengine 11 wamehukumiwa miaka 15 huku mtu mmoja alichukumiwa miaka 30.
Ameeleza kwamba tangu wamehukumiwa kifungo hicho ndugu hawajawahi kuruhusiwa kuwaona na hawajui wamefungwa gereza gani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tauzakta Mkoa wa Morogoro Sheikh Juma Kitungu amebainisha kwamba tangu kise hiyo imeanza na hadi kufikia hukumu alifanya upelelezi wake na kibaini Ukweli wa tuhuma hizo.
Amebainisha kwamba tuhuma hizo ni za kubambikiwa kwani kesi hiyo imegubikwa na ushahidi wa uongo.
“Naomba nikuteni na Rais kuna jambo nataka nimweleze, kuna mambo ya uongo na kuna ushahidi wa uongo kweli kesi hii,” amesisitiza Sheikh Juma.
Naye ndugu wa momja wa wahukumiwa Nurdin Sultan amesema kwamba wanamaumivu makubwa kwa namna ndugu yake alivyokamatwa.
Hivyo amemuomba Rais Dkt. Samia kuwasaidia ili waweze kuwaona kama wako hai na hata kama hawako hai wakabidhiwe miili ya ili wakaistili.
No comments