DIWANI PAZI; SERIKALI IMEDHAMIRIA KUBORESHA ELIMU KUPITIA TEHAMA
Dar es salaam:
Diwani wa Kata ya Buguruni, Busoro Pazi amesema serikali kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) imedhamiria kuimarisha elimu kupitia mifumo ya tehama katika kata hiyo.
Akizungumzwa katika mahojiano na mwandishi wa mtandano huu kuhusu utekelezaji wa ilani ya CCM katika kuwaletea maendeleo wanabuguruni.
“Tunavyo vipaumbele vingi lakini tunawekeza zaidi kwenye elimu ya tehama haswa mimi katika jimbo langu nimepania kufanya makubwa katika sekta ya elimu ambapo kwasasa nipo katika mazungumzo na baadhi ya wadau ambao tunajipanga kutoa mafunzo ya tehama kwa walimu wa shule zote za serikali katika kata yetu” alisema
Pazi alisema amewiwa kufanya hivyo kwakuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CCM Taifa amegawa vishikwambi kwa walimu wote nchini vilivyotumika katika sensa ya watu na makazi 2022 lakini havitumiki kama ilivyokusudiwa.
“Mwandishi nikuambie ukweli vishikwambi kweli walimu wetu nchi nzima wamepatiwa lakini matumizi makubwa yanayotumika zaidi ni ya mawasiliano ya kawaida ambayo ni mawasiliano kama simu ya mkononi, matumizi ya picha za video, mnato na mitandao ya kijamii kama whatsap, Instagram, barua pepe, badoo na matumizi mengineyo” alisema Pazi
Aidha Pazi alisema hapingani na matumizi hayo lakini ni kiu kubwa na shauku ya Rais Dk Samia kuona Vishikwambi hivyo vinakuza taaluma shuleni na ndiyo maana sasa anaamua kutoa mafunzo na kufunga mifumo ya tehama kwa shule zote za kata ya buguruni.
Pazi alitanabaisha wazi jinsi mfumo wa mawasiliano uliofungwa shule ya msingi Bunguruni na baadhi ya shule katika kata hiyo unavyowanufaisha walimu ambao umefungwa na kampuni ya mawasilino ya tehama ‘kuonana kona Ltd
Achilia mbali huduma ya elimu katika kata hiyo, Pazi aliliambia HabariLEO bado hajaiona Buguruni aipendayo na hivyo kuahidi kufanya makubwa kwa ushirikiano wa wananchi na chama anachokitumikia.
“Mengi yamefanyika kwa miaka miwili ya Rais Samia lakini bado tunahitaji kufanya makubwa zaidi sasa hivi tunatarajia kujenga kituo cha kisasa cha afya kata ya Buguruni maana hatuna kituo kilichokuwa cha Buguruni kimebaki Kwa mnyamani ambapo kwa sasa siyo kata ya Buguruni, ujenzi wa soko la kisasa na Barabara zinazozunguka mitaa ya buguruni itakuwa ya kisasa zaidi ikimulikwa na taa usiku” alisema
Katika ujenzi wa kituo cha afya tayari wakazi watakaopisha ujenzi wa hospitali katika maeneo yao tayari wameshaanza kulipwa fedha zao na Sh 244milioni zimeratibu mpango wa fidia kwa wakazi watakao pisha ujenzi wa kituo cha afya.
Baadhi ya wakazi wa Buguruni wakiwemo wafanyabiashara wa soko la Buguruni walisema chini ya uongozi wa Pazi wameona maendeleo.
“Naitwa Haroun Shaibu muuzaji wa Samaki Sokoni hapa, kwa miaka miwili tumeona maboresho makubwa ya soko ikiwemo usafi na miundombinu nah ii ni kutokana na uongozi safi na siasa bora zinazosimamia soko hili bila siasa bora hakuna Maisha bora wala uchumi imara” alisema Shaibu
Kwa upande wake mamalishe wa soko la Buguruni Fatma Saidi alisema Pamoja na mazuri yanayofanywa na Diwani na Mbunge wa jimbo la Segerea bado mpango maalumu unahitajika kuwaelimisha wafanyabiashara na kuwapanga vizuri katika eneo linalozunguka soko.
“Tunaona mafanikio sawa lakini kuna mambo hayapo sawa kuna wakati tunaamani hususani tunaopanga vitu nje ya soko na kuna wakati hatuthaminiki uongozi wa soko waweza amua muda wowote kumarisha mgambo wa jiji kutuondoa hapa kutupeleka kule ni tafrani pasipo sababu huku wakichukuwa ushuru” alisema
No comments