WEKEZA LINDI KWA UKUAJI WA UCHUMI NA MAENDELEO SEKTA YA MADINI
Maonesho ya Kwanza ya Madini yanayoendelea wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi katika Viwanja vya Kilima Hewa yaliyobebwa na Kaulimbiu ya isemayo "Wekeza Lindi kwa Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya Jamii yameendelea kutembelewa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini pamoja na wananchi wa Mkoa huo.
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) inaendelea kutoa elimu ya taarifa za tafiti za Madini mbalimbali yapatikanayo nchini Tanzania kilichotolewa Mwaka 2023.
Akizungumza katika maonesho hayo, Meneja wa Sehemu ya Jiolojia Maswi Solomon amesema GST imejipanga kusambaza vitabu vinavyoanesha Madini yapatikanayo Tanzania kwa Wakuu Mikoa na Wilaya kote nchini zoezi linaloenda sambamba na uelimishaji wa masuala mbalimbali ya jiolojia na madini katika Mikoa husika.
Pamoja na mambo mengine, Maswi ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini kufika katika Banda hilo ajili ya kujipatia nakala ya Kitabu cha Madini pamoja na kujipatia elimu na muongozo wa tafiti zilizofanyika nchini ikiwemo uchunguzi na utambuzi wa sampuli za Madini, Uchenjuaji, na elimu ya tabia za miamba.
Katika hatua nyingine, Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kinaendelea kutangaza bidhaa na huduma zake ikiwemo vidani, Pete, vikuku, mikufu, hereni pamoja na nafasi za mafunzo ya uongezaji thamani wa madini ya vito ambapo wadau mbalimbali wanaendelea kutembelea banda hilo kwa ajili ya kuchukua fomu za kujiunga na chuo hicho.
TGC inatoa mafunzo mbalimbali ikiwemo Ukataji wa Madini na Ung'alishaji wa Madini ya Vito, Usonara na utambuzi wa Madini ya Vito.
No comments