MAWAKILI WAUNGA MKONO MKATABA UBORESHAJI WA BANDARI KATI YA TANZANIA NA DUBAI

Mwenyekiti Mawakili Wazalendo, Bwana Juma Nassoro alifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari kuunga mkono baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendelezaji na uboreshaji wa bandari Tanzania jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam:
Mawakali Wazalendo wameeleza kuwa wanaunga mkono makubaliano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu uendelezaji na uboreshaji wa bandari Tanzania.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti Mawakili Wazalendo, Bwana Juma Nassoro amesema katika makubaliano hayo serikali imefanya jukumu lake kwa kutekeleza mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa katiba, sheria na desturi zinazotawala.

“Baada ya kufanya majadiliano, makubaliano yaliandaliwa na kusainiwa. Ibara ya 31 ya Makubaliano inahitaji makubaliano hayo kuridhiwa. Na hapa kwetu wenye mamlaka ya kuridhia ni Bunge chini ya Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”. Alisema Wakili Nassoro na kuongeza,

“Bunge ndicho chombo ambacho kina wawakilishi wa wananchi. Na Bunge limeridhia makubaliano hayo baada ya kujadili kwenye vikao vyake na kuridhika kuwa makubaliano hayo yana manufaa makubwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”.

Hivyo amesema Serikali imetimiza wajibu wake na itaendelea kusimamia utekelezaji wake kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi.

“Nasi tunaunga mkono juhudi hizo za Serikali za kutafuta wawekezaji kutekeleza sera na sheria za nchi, tunaunga mkono na kupongeza hatua ya Serikali kutafuta ridhaa ya Bunge na kuruhusu mjadala wa wazi na maoni ya wananchi,” Alisema wakili Nassoro

Sisi mawakili wazalendo Tunatambua utekelezaji wa makubaliano haya hayajaanza, kuna hatua kadhaa za kitaalam na kiufundi zitafuata. Watanzania hatuna sababu ya kutilia shaka utekelezaji wa makubaliano hayo

Amesema kuwa vipengele vinavyoleta mjadala, vimetafsiriwa vibaya aidha kwa makusudi yaliyojificha au bila kujua.

Ameeleza baadhi ya vifungu hivyo kuwa ni kuhusu ukomo wa muda wa makubaliano, bandari zitakazohusika, uhalali wa serikali ya Dubai kuingia makubaliano, umiliki wa ardhi, mtazamo wa sheria kuhusu makubaliano kuridhiwa na Bunge, mtazamo wa sheria kuhusu Serikali kusaini makubaliano na baadaye na Bunge na Faida za kuingia makubaliano.

No comments