UVCCM: HALMASHAURI ZOTE NCHI ZIANDAE MKAKATI WA KUWATAFUTIA FURSA VIJANA
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM) umewataka viongozi wa halmashauri na mikoa yote nchini kuwatafutia fursa za vijana ili weweze na kujikwamua kiuchumi.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi (UVCCM) Taifa Edna Lameck juu ya ziara ya umoja huo iliyoanza tarehe 11-8-2023 yenye lengo kukutana na vijana na kuwasikiliza changamoto zao.
“Tunawaomba Viongozi wa serikali kuhakikisha vijana wanapewa sehemu za kufanyia Biashara na badala ya kusema vijana wajiajiri halafu haujawawekea mazingira ya kujiajiri”Alisema Bi. Edna.
Alisema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania dokta Samia Suluhu Hassan ameshatoa fursa kwa vijana ikiwemo kuelekeza pesa za mikopo za vijana huku wakiwataka viongozi waige mfano wake.
Akizungumzia Ziara hiyo amesema katika ziara hiyo wamebaini bado kuna changamoto kwa vijana wa Bodaboda katika kujitafutia Riziki.
“Vijana wa Bodaboda bado wanazo changamoto ya kutopata vibali vya kufanyia kazi zao tunaomba mamlaka husika wawatafutia vijana hawa maeneo ya maalum hili waweze kufanya shughuli zao”Alisema Bi. Edna.
Katika hatua nyingine Bi. Edna ametoa wito kwa vijana wote wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani kujitokeza kesho katika mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Mbagala zakhem siku ya kesho Jumapili Agost 27 mwaka huu.
No comments