TMA KUTOA HUDUMA MAHUSUSI NEEMA KWA WAKULIMA

Mbeya;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale, Uyole –Mbeya, kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2023.

Akizingumza katika maonesho hayo Meneja wa Huduma za Hali ya Hewa Kilimo, ndg. Isack Yona
amewakaribisha wananchi na wakulima kufika bandani hapo ili kupata elimu ya hali ya 
hewa pamoja na kufahamu umuhimu wa kutumia huduma hiyo mahususi katika maeneo yao.

“Magonjwa mengi yanayoshambulia mazao yatategemea hali ya hewa, kwa mfano hali ya baridi husababisha mazao kuchelewa kukomaa, lakini sasa kupitia huduma hizi mahususi itakuwa neema kwa wakulima,
tutamfungashia kadri anavyohitaji yeye ili apange namna ya kukabiliana na hali tarajiwa katika eneo alilopo” alisisitiza Ndg. Isack Yona.

Aidha, Kaimu Meneja -TMA Songwe, ndg. Abel Nyamenda ameelezea kuwa kwa sasa TMA inatumia teknolojia ipasavyo katika kutoa huduma bora kwa wateja wake, hivyo ni vyema wadau kuzitumia huduma hizo ili kuleta tija katika sekta zao.

Kwa upande mwingine wananchi waliotembelea bandani hapo waliomba 
Mamlaka kujenga ofisi zao huko vijijini ili mkulima anapohitaji huduma hizo 
mahususi iwe rahisi kuzipata kwa wakati zikiwa sahihi ili kuhepusha kuwekeza katika kilimo na kupata hasara. 

No comments