ACTIVE MAMA MKOMBOZI WA WAKULIMA WA NAZI MKOA WA PWANI
Na Mohamed Mussa
Wakina mama mbalimbali kutoka mkoa wa pwani wamesema wamekuwa wakinufaika na kilimo cha nazi baada ya wawekezaji wengi kuwekeza katika bidhaa ya nazi na kufanya kilimo hicho kupanda thamani.
Akizungumza na katika mahojiano naalumu na mwandishi wa mdandao huu juu ya namna wanavyoendesha biashara hiyo mfanyabiashara wa kuuza na kubangua nazi Bi. Khadija Mohamed amesema zao hilo limekuwa likipata umaarufu mkubwa kutokana na watu wengi kutumia mafuta ya nasi hususani mijini hasa kujipakaa.
Alisema anamshukuru sana mkurugenzi wa Active Mama, Ernestina Mwenda ‘Cocunut Lady’ kutokana na kuwaunga mkono kwa kununua nazi nyingi ambazo zinawasaidia katika kujikimu katika maisha yao ya kila siku.
Alisema kampuni ya Active Mama imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia wakinamama kwa kununua nazi katika maeneo yao na kufanya ubanguaji wa nazi hali ambayo imewapa ajira mara mbili.
“Kwanza tunauza nazi ambapo tumekuwa tukipata fedha za kutosha, lakini pia amekuwa akibangua nazi na kufanya tupate ajira nyingine”Alisema Bi. Khadija.
Bi. Khadija ameongeza kuwa wamekuwa wakitumia nazi za asili kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ya Active Mama kama sehemu ya kuunga mkono kilimo cha nazi lakini pia kuifanya jamii kutotumia kemikali katika miili yao.
“Unapotumia mafuta ya nazi ya asili, unafanya ngozi yako ibaki katika ubora unaostahili, lakini pia unasaidia kilimo cha nazi kwa ndani ya nchi" Alisema
No comments