BONGO FIGHTING CHAMPIONSHIP KUFANYIKA JULY 29 JIJINI DAR
Uzinduzi wa Pambano la mchezo wa mchanganyiko wa karate Bongo Fighting championship (BFC) umefanyika rasmi ambapo pambano hilo litafanyika July 29 katika ukumbi Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Super Dome na muandaaji mwenza wa pambano hilo Patrick Farrell amesema pambano hilo ni sehemu ya mapinduzi makubwa ya mchezo wa mchanganyiko wa karate na ndondi hususani katika ukanda huu wa afrika ya mashariki.
"Wote mmeona mafanikio ya vyombo vya habari vya michezo kwa mabilioni ya dola katika michuano ya UFC na One, sasa ni wakati wa Tanzania kuzindua toleo lake la Afrika Mashariki la ukuzaji wa taaluma mchanganyiko ya karate na ndondi” Alisema Bw. Farrell
Alisema siku hiyo yatafanyika jumla ya mapambano kumi na tatu kwa usiku mmoja, ambapo mapambano ya ngumi za kulipwa saba na mtaalamu sita wa Muay Thai, akiwemo raia wa kwanza wa WBC Muay Thai kwani Usiku huu wa mapambano ya bila kufungana utakuacha ukitaka zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Dragon Promotions bwana Ricky Agayas amesema Ni wakati wa kuonyesha baadhi ya ari ya mapigano ya Tanzania katika ukanda wa huu wa Afrika Mashariki na kati.
"Huu ni wakati wa kuonyesha ya Ari ya mapigano ya Tanzania Afrika Mashariki na kati hivyo kupitia ushirikiano na Super Dome na Kasino ya Palm Beach kuandika historia mpya katika mchezo huu" Alisema Bw. Agayas.
Bongo Fighting championship imendaliwa kwa ushirikiano wa Superdome ikishirikiana na Dragoni Promotion, Palm Beach, Piga bet na Grand Casino.
Kwa upande wa matangazo ni Palm Beach Casino, Le Grande Casino, Pigabet, Pepsi kupitia kinywaji cha Supa Komando, Hill Water na Sper Dome pamoja na TV3 inayopatikana kupitia king'amuzi cha StarTimes na Clouds Media
Alisema tiketi za usiku huo wa Pambano la Bongo Fighting championship (BFC) zinapatikana Aplikesheni ya Nlipe.
No comments