Breaking News

WAZAZI WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA MALEZI BORA HILI KUTOMOEZA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA

Msaidizi wa kiongozi mkuu wa Jumuia ya Tanzania Ithnashariyya Community (TIC), Sheikh Mohammad Abdi akiwasilisha mada katika Kongamano Maalum la Kupinga Ukatili wa Kijinsia, lililofanyika katika Ukumbi wa TIC Makamo Makuu Kigogo Post Dar es salaam
kamanda wa Polisi mkoa wa kinondoni ACP  Ally Wendo akifafanua jambo wakati wakiwasilisha mada katika Kongamano Maalum la Kupinga Ukatili wa Kijinsia, lililofanyika katika Ukumbi wa TIC Makamo Makuu Kigogo Post Dar es salaam.
Washiriki wakifatilia mada zinazo wasilishwa katika Kongamano Maalum la Kupinga Ukatili wa Kijinsia, lililofanyika katika Ukumbi wa TIC Makamo Makuu Kigogo Post Dar  es salaam
Afisa mwandamizi kutoka dawati la jinsia jeshi la polisi, Dokta Yatosha akizungumza katika Kongamano Maalum la Kupinga Ukatili wa Kijinsia, lililofanyika katika Ukumbi wa TIC Makamo Makuu Kigogo Post Dar es salaam.

Dar es Salaam:
Jamii imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii kwa kushiriki katika malezi bora na kutoa elimu juu ya maswala hayo.

Akizungumza katika kongamano liloandaliwa na Jumuia ya Tanzania Ithnashariyya Community (TIC) la 
Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Afisa mwandamizi kutoka dawati la jinsia jeshi la polisi, Dokta Yatosha  Lukindo  amesema jamii inayo nafasi kubwa hasa katika kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa nchini.

"Matukio haya yamekuwa yakitokea kutokana jamii yenyewe na viongozi husani wa kidini kutokutoa mchango stahiki wa kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vinapigwa vita na kukemewa na kila mmoja katika jamii" Alisema Dk Lukindo.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa chanzo cha kuongezeka kwa matukio ya  haya ya Ukatili wa Kijinsia ni Ugumu wa maisha, kukua kwa teknolojia pamoja na jamii kutokuwa na hofu ya Mungu.

Mapema akiwasilisha mada juu ya lengo ya kongamano hili msaidizi wa kiongozi mkuu wa Jumuia ya Tanzania Ithnashariyya Community (TIC), Sheikh Mohammad Abdi amesema wameandaa kongamano hili kwa kutambua nafasi yao wao kama vingozi wa dini na mchango wao mkubwa katika kuhakikisha kuwa tunatokomeza vitendo hivyo.

"Viongozi wa dini tunayo nafasi kubwa ya kuhakikisha tunashiriki katika kutoa elimu kwa waumini wetu juu ya madhara ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii yetu" Alisema Sheikh Abdi.

Kwa upende wake kamanda wa Polisi mkoa wa kinondoni ACP  Ally Wendo amesema matukio mengi ambayo yameripotiwa yanaonyesha waanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia wengi utendewa matukio hayo na watu wa karibu katika familia zao.

"Kwa mujibu wa matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa kuonyesha kuwa yanafanywa na watu wa karibu ndani ya familia husika ikiwemo ndugu wa karibu" Alisema ACP Wendo.

Alisema jeshi la polisi limekuwa likichukua hatua mbaliambali kuhakikisha linatokomeza matukio haya katika jamii kwa kuanza mpango kutembelea jamii na kuzungumza nayo kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kujenga 
ushirikiano.


Washiriki wakifatilia mada zinazo wasilishwa katika Kongamano Maalum la Kupinga Ukatili wa Kijinsia, lililofanyika katika Ukumbi wa TIC Makamo Makuu Kigogo Post Dar  es salaam

No comments