Breaking News

TUZO YA HARUSI KUFANYIKA MEI 28 JIJINI DAR

Msimu wa tatu wa Tuzo za Harusi umezinduliwa rasmi ambapo kwa mwaka huu zitafanyika siku ya tarehe 28 Mei katika hotel ya The Kilimanjaro Hotel.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huo kwa niaba ya waandaaji wa wa Tuzo hiyo Bwana Benedict Msofe amesema kwa kipindi cha miaka minne ya kufanyika kwa maonyesho hayo kwa mafanikio makubwa mwaka huu yameboreshwa zaidi.

"Ni miaka minne sasa tangu kuanza kufanyika kwa maonyesho ya biashara ya harusi, kutokana na mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kipindi hicho na kwa kuzingatia maoni mazuri kutoka kwa wadau imepelekea kuona upo ulazima wa kuandaa tuzo za harusi" Alisema Bw. Msofe

Alisema tuzo hizo mabazo kwa mwaka huu zinafanyika kwa mara ya tatu ambapo kwa mwaka huu itakuwa na vipengele 21 ambapo vipengele 19 uteuzi ulikuwa wazi kwa umma ambao ulifunguliwa January 20 ambapo zaidi ya majina 340 yalipokelewa kutoka kwa vikundi 19 kupitia mitandao yetu ya kijamii pamoja na ujumbe wa simu.

Aidha bw. Msofe aliongeza kuwa washiriki watapiguwa kura badae jopo la wachambuzi wa sekta ya harusi watazipitia kazi za washiriki wote kwa lengo la kuangalia ubora na ubunifu katika kazi zao.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka kampuni ya Innovex Tanzania Miss Bahiya Tajiri amesema kwa mwaka wa pili mfululizo tumekuwa sehemu ya kuandaa tuzo za harusi kwa kuhakikisha kuwa ubora wa kura zinazopigwa katika kipindi chote cha zoezi la upigaji kura.

"Sisi tumekuwa bega kwa bega kuhakikisha kuwa kura zote zinazopigwa zinakuwa na ubora kwa kuamini kuwa tuzo hizi zina tija kubwa katika jamii yetu hivyo kuhakikisha kuwa kura zote zinazopigwa zinakuwa huru na haki" Alisema Bi Tajiri.

Tuzo za mwaka huu jumla ya catalogi 19 zitashindindaniwa ambazo ni ukumbi bora wa harusi wa mwaka, mwokaji bora wa keki, mtaalam wa maua, mpishi bora, mtengeneza vitafunwa bora, mtengeneza nywele na mwanamitindo bora, saluni bora.

Amezitaja nyingine kuwa ni mshereheshaji (MC) bora, DJ wa harusi bora,muuza vifaa bora vya harusi, duka la vifaa vya harusi, duka la nguo za harusi (kike), muuza viyi vya harusi bora, mchoraji wa henna bora, mbunifu wa nguo za kiume bora na tuzo ya heshima hutolewa kwa harusi bora ya mwaka pamoja na tuzi ya mafanikio ya mtu binafsi na taasisi ilioacha alama kwenye sekta harusi.  

No comments