Breaking News

MWENYEKITI JUMUIYA YA WANAWAKE CUF TAIFA AHAMIA ACT WAZALENDO


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CUF, Ndugu Kiza Mayeye akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhamia chama hicho akitokea chama cha CUF.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Act Wazalendo Taifa, Ndugu Dorothy Semu akimkabidhi kadi ya uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CUF, Ndugu Kiza Mayeye mara baada ya kujiunga na chama hicho.

Dar es salaam
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CUF (JUKE) taifa na Mbunge wa Viti Maalum, Bi.Kiza Mayeye amejiondoa kwenye Chama cha CUF na kujiunga rasmi na chama cha ACT Wazalendo.

Akizungumza mara baada ya kupewa kadi ya uanachama mpya wa makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam amesema tayali nimekwishajisajili katika mfumo wa kuandikisha wanachama wa ACT Kiganjani, na kulipia aina ya kadi ya Maalim Seif.

"Leo Mei 23 tayali nimejisajili katika mfumo wa kuandikisha wanachama wa ACT Kiganjani, na kulipia aina ya kadi ya Maalim Seif kwa ada ya uanachama kwa miezi sitini (miaka mitano) Hivyo kuanzia leo mimi ni mwanachama kamili wa ACT Wazalendo" Alisema Bi. Mayeye

Alisema katika kipindi cha miaka kumi na tatu amekitumikia Chama cha CUF kwa nafasi mbalimbali tangu mwaka 2011 nilipojiunga nacho. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipokishukuru Chama cha CUF kwa kunilea kiuongozi na kunipa fursa mbalimbali kukitumikia.

Bi. Mayeye alimezitaja sababu zilizomlazimisha kuchukua maamuzi haya magumu kuwa yeye ni mwanasiasa wa vitendo, na kull
amini siasa halisi ipo chini (field), kwa wananchi.

"Mwaka 2020 niligombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini na kwa matokeo halisi nilishinda. Lakini, kilichotokea mwaka 2020 sote tunakifahamu; walioshinda walishindwishwa na walioshindwa walishindishwa" Alisema na kuongeza kuwa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipotangaza kuwa nimekuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 16252 kila mmoja alishangaa! Bila shaka hata CCM wenyewe walishangaa, kwa sababu walijua nilishinda!

Alisema ninajiunga ACT Wazalendo ili kuendeleza mapambano. Nimefanya uchambuzi wa kina na kujiridhisha kuwa ACT Wazalendo ndio jahazi sahihi la kuendeleza harakati zangu kwa ajili ya kuwakomboa wanachi wa Kigoma Kaskazini, Mkoa mzima wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.

Nimevutiwa sana na sera za ACT Wazalendo za kujenga Tanzania ya wote kwa maslahi ya wote. Nimeshawishika pia na jitihada za Chama kuimarisha mtandao wake nchi nzima. Nimevutiwa pia na jitihada za Chama kukuza vipaji vya vijana na wanawake.

Kabla sijafanya uamuzi huu nimezungumza na vyama vingi ili kufanya utafiti kabla ya kujiunga na Chama husika. Mwishowe nikafanya hitimisho kuwa ACT Wazalendo ndio jukwaa sahihi. Wale ambao walitarajia nitajiunga nao, waniwie radhi, vigezo vya kisayansi vimenipeleka ACT Wazalendo!

Nimekuja kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa Chama katika kujihakikishia ushindi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Ninatarajia kwenda Jimboni Kigoma Kaskazini hivi karibuni. Huko nitaeleza kwa kina zaidi kwa nini Chama hiki kinapaswa kuwa tumaini lao kutokana na utafiti na  uchambuzi wa kina nilioufanya

No comments