ITEL TANZANIA YATOA MSAADA KITUO CHA KULELEA WATOTO CHA CHAKUHAMA JIJINI DAR
Meneja masoko mkoa wa Dar es Salaam, bwana Shaibu Jeremiah akiwa katika picha ya pamoja mara baa ya kukabidhi msaada kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha CHAKUAHAMA jijini Dar es salaam
Meneja masoko mkoa wa Dar es Salaam, bwana Shaibu Jeremiah akifafanua jambo katika hafla ya kutoa msaada kwa watoto wanaishi katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha CHAKUHAMA jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Kampuni ya simu ya Itel Mobile Limited imetoa msaada wa Vyakula na vifaa vya shule kwa kituo cha kulelea watoto wanaotoka katika mazingira magumu cha CHAKUHAMA kilichopo sinza jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi misaada hiyo, Meneja masoko mkoa wa Dar es Salaam, bwana Shaibu Jeremiah amesema lengo la kutoa msaada huo wenye thamani ya shilingi million 5 ni kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha kunakuwepo na mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi mashuleni.
"Hakuna asiyefahu kuwa watoto ni hazina na ni taifa la lijalo, Itel kupitia kupitia kauli mbiu yetu ya "Enjoy Better Life" tumekuwa tukisaidia wanafunzi/ watoto hasa wanatoka katika mazingira magumu kwa kuwasaidia kuweza kuwa na mazingira mazuri ya kujisomea au vitendea kazi mashuleni" Alisema Bw.Jeremiah
Alisema kupitia program hiyo, Itel Tanzania imekuwa wakitoa misaada ambayo itasaidia kutengeneza mazingira bora lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nao kufurahia maisha ikiwa ni pamoja kuwawekea na mazingira bora ya kujisomea.
"Kupitia program yetu ya CSR ambayo imeanzishwa mwaka 2003 imekuwa ikirudisha fadhila kwa jamii na imekuwa ikitekelezwa katika nchi zote za afrika ambazo Itel inapatikana" Alisema Bw. Jeremiah.
Bw Jeremiah aliongeza kuwa kupitia program hiyo Itel Tanzania tayali wameanzisha mradi mbalimbali nchini katika shule za watoto wanaishi katika mazingira magumu ikiwemo mradi ya maktaba unaojulikana kama "wandering libraries project" ambao utachangia maktaba ndogo zaidi ya 10,000 kote barani afrika katika kipindi cha miaka 3.
Nae mlezi na msimamizi wa kituo hicho ameishukuru kampuni ya Itel Tanzania kwa msaada huo kubwa kwan umekuja wakati sahihi na kuhaidi kutumia kama ilivyokusudiwa
Baadhi ya watoto wakifurahia msaada waliopatiwa na kampuni ya ITEL Tanzania katika hafla iliyofanyika katika kituo hicho jijini Dar es salaam.
No comments