Breaking News

SHEIKH JALALA HAIMIZA UMOJA NA MSHIKAMANO, AKEMEA VITENDO VYA SHOGA

Kiongozi wa dhehebu la Waislam Shia Ithnasheriya, Maulana Sheikh Hemed Jalala akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari katika matembezi ya siku Quds yalioanzia ilala mpaka Masjid Ghadir Kigogo Post Dar es salaam.

Dar es salaam:
Jamii imetakiwa kuendelea kuenzi na kutunza tunu ya amani, umoja na mshikamano iliyopo nchini ikiwa ni moja ya tunu hii Adhimu ambayo tumejaaliwa na kufundishwa na mafundisho ya madhehebu yote ya dini ikiwemo ukristo na uislamu.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na Kiongozi wa dhehebu la Waislam Shia Ithnasheriya, Maulana Sheikh Hemed Jalala wakati wa matembezi ya kumbukumbu ya siku ya Quds ambayo ufanyika kila ijumaa ya mwisho wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

"Siku hii adhimu nyenye lengo la kuenzi na kupaza sauti juu ya amani, umoja na mshikamano kwa uislam na wasio waislam pamoja na kukumbuka madhila yanayoendelea duniani kote hususani katika ardhi ya Palestina " Alisema Sheikh Jalala.

Alisema siku Quds ni siku ambayo inawaleta pamoja waislam na wakristo pia ni siku ya kukumbuka madhila wanayoyapata taifa la palestina.

Sheikh Jalala aliongeza imekuwa ikiubili na kutangaza juu ya kuleta umoja kati ya waislam na wakristo , waislam na wayahudi kutokana na kukusanya dini zote pamoja na kupaza sauti kuimiza umoja, hasa katika ardhi ya Palestina katika mji wa Yerusalem mambapo ndio makao makuu ya dini zote mbili.

Katika hatua nyingine kiongozi huo amewataka wazazi na walezi kujikita zaidi katika kuela vojana kwa kufata misingi na mafundisho ya dini kutokana na kuenea kwa janga la ushoga na usagaji.

"Nitoe rai kwa wazazi na walezi kuela vijana wao kwa kufata mafundisho ya dini zetu kuhakikisha kuwa wanawalinda na janga hili la ushoga na usagani" Alisema Jalala


No comments