Breaking News

RC KUNENGE: WATANZANIA TUJIVUNIE MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza wakati  akifungua kongamano la miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani pwani 24 April 2023.
Mzee Ngemela Lubinga akichangia mada katika kongamano la kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani pwani 24 April 2023.
Bibi Mtolo Katele akifafanua jambo wakati akitoa mada katika kongamano la kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani pwani 24 April 2023
Mzee Jumanne Mangara kitoa mada katika kongamano la kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani pwani 24 April 2023.

Kibaha - PWANI
Mkuu wa Mkoa wa Pwani mheshimiwa Abubakar Kunenge amewataka Watanzania kujivunia na kuulinda muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kunenge ametoa Kauli hiyo leo Aprili 24, 2023 Mkoani Pwani akifunguka kongamano la miaka 59 ya Muungano huo lililofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere.

Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kwamba yapo mataifa mengi na makubwa ambayo yameshindwa kudumisha Muungano wao lakini Muungano huu umedumu na kuwa wa mfano.

“Ni jambo la kujivunia hadi sasa kuwa na Muungano huu, mataifa mengi na makubwa yameshindwa kuungana,” amesema RC Kunenge na kuongeza,

“Hivyo tunajivunia kuwa na Muungano huu, kwani ni Muungano wa kihistoria, tumeona mataifa mengine yakitumia njian nyingine za kuungana ikiwemo kuanzia kiuchumi na kadhalika,”.

RC Kunenge ametumia fursa hiyo kuongeza Awamu zote za Serikali zilizopita kwa kuulinda na kuudumisha Muungano huu hususan kipindi hiki cha utawala wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejipambanua katika kutatua kero za Muungano.

Kadhalika Kunenge amesema ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha analinda na kuutunza Muungano huu.
Picha za matukio mbalimbali katika  kongamano la kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani pwani 24 April 2023.






No comments