Breaking News

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YAKAMILIKA, MSAMA ATAMBA KUWEKA HISTORIA KESHO

Mkurugenzi wa Msama Promotion Bwnana Alex Msama akifafanua jambo kwa na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya Tamasha la pasaka litakalofanyika 9 April 2023 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bwnana Alex Msama akiwaonyesha waandishi wa habari jukwaa litakalotumika Tamasha la pasaka litakalofanyika 9 April 2023 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam:
Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama ambaye ndiye muandaaji wa Tamasha kubwa la Pasaka amesema maandalizi ya tamasha hilo ambalo ufanyika kila mwaka yamekamilika kwa asilimia mia ambapo mwaka huu linatarajiwa kuwa na viwango vya kimataifa kwa limeboreshwa zaidi kwa kuwa na viwango vya kimataifa

Akizungumza mara baada ya kukagua maandalizi Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 kuanzia ufungwaji wa jukwaa la kisasa, vyombo vyaa mziki, eneo la michezo ya watoto pamoja na waimbaji wa Injili wa Kimataifa wa kimataifa ambao watatumbuiza siku ya tamasha hilo kuwa wote wameshawasili nchini.

Alisema Tamasha la mwaka huu pamoja na maboresho yaliyofanyika na kulifanya kuwa na viwango vya kimataifa alitakuwa na kiingilio ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, ambaye atakiwa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tamasha la mwaka huu litakuwa la kihistoria kutokana na maboresho yaliyofanyika pamoja na kuwa mahususi kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Pasaka pia tutaadhisha  miaka miwili ya Rais Dkt. Samia tangu kuingia madarakani” Alisema Bw. Msama.

Aidha Msama amewataka watanzania na wapenzi wa nyimbo za injili kutoka mkoa wa dar es salaam na mikoa ya jiranu kujitokeza kwa wingi 9 April siku ya tamasha hilo kushuhudia waimbaji wakali wa nyimbo za injili wakitumbuiza na amesisitiza kuwa halitakuwa na kiingilio.

“Tamasha la mwaka hili halitakuwa na kiingilio litakuwa bure, tunawaomba wanachi wa mkoa wa dar es salaam na mikoa jirani kujitokeza siku ya tarehe 9 april katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni kwa ajili ya kumsifu Mungu,” Alisema Msama.

Pia amewahakikishia wananchi wote watakao fika siku hiyo.kuwepo kwa ulinzi wa kutosha kwan jeahi la polisi kinondoni limeaidi kuimalisha ulinzi kwa wananchi na mali zao.

No comments