Breaking News

COSTECH YAENDESHA WARSHA YA KUONGEZA THAMANI YA BUNIFU, WASHIRIKI WAKIONYESHA UBUNIFU

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Intermech Engineering Limited Mhandisi Peter Chisawillo akielezea juu ya mashine hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Mtaalam wa Mashirikiano kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Bi. Promise Mwakale akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam
Kampuni ya Intermech Engineering Limited iliyopo mkaoni Morogoro imesanifu, kubuni na kuunda mashine ya kukausha muhogo.

Akizungumza katika warsha ya kuongeza thamani bunifu za hapa nchini iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) kwa ufadhili wa Taasisi ya FUNGUO Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mhandisi Peter Chisawillo katika warsha mashine hiyo itasaidia kuongeza thamani ya zao hilo.

Amesema mashine hiyo imevumbuliwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Greenwich cha nchini Uingereza na kutengenezwa na Kampuni hiyo kwa ufadhili wa COSTECH.

“Kazi yetu ni kusanifu, kubuni na kuunda mashine za kusindika mazao ya kilimo, na kwa sasa tumekuja na mashine ya kukausha muhogo, “Flush Dryer” ambayo umevumbuliwa kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Greenwich cha nchini Uingereza na kutengenezwa na kiwanda chetu” Alisema Mhandisi Chisawillo

Mhandisi Chisawillo alibainisha kuwa mashine hiyo inauwezo wa kukausha tani saba za muhogo kwa siku ambayo ni sawa na kilo 2100 za muhogo.

Pia Mhandisi Chisawillo ameeleza kuwa ufumbuzi wa mashine hiyo umekuja kufatia kuwepo na changamoto ya kuharibika haraka kwa zao hilo muhimu, hivyo kuamua kuja na mashine hiyo ambayo itasaidia kukausha haraka na kuzuia kuharibika.

Kwa upande wake Mtaalam wa Mashirikiano kutoka COSTECH, Bi. Promise Mwakale amesema lengo la Warsha hiyo ambayo imewaleta pamoja wadau ni kuongeza thamani ya bunifu za hapa nchini.

Alisema kwa ushirikiano wa Vyuo tunaweza kukuza thamani hiyo ya bunifu ambapo hadi sasa ilishabuniwa na kutengenezwa unga usio na sumu kuvu.

Aliongexa kuwa kupitia ushirikiano na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela tayali umesaida kubuniwa kwa Teknolojia ya Magamba ya kutengenezea ngozi nzuri na bora.

Hii inaonyesha kuwa ni dhahiri Vyuo vinaweza kusaidia kubuni teknolojia ambazo zinaweza kuongeza tahamani ya bidhaa zetu.

No comments