Breaking News

COSTECH YAADHIMISHA WIKI YA UBUNIFU

Katika kuhakikisha kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu kinakata kiu ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam na kutumika kama jukwaa la kutangaza bidhaa za kitafiti na bunifu kwa wajasiriamali, Wabunifu na Taasisi mbalimbali kutumia fursa hiyo adhimu ya kujitangaza na kubiasharisha bidhaa hizo ili ziweze kuwafikia wananchi na kuwaletea maendelo kwa haraka kiuchumi na kijamii nchini.

Wiki hiyo inaendelea kuadhimishwa kwa siku tatu (3) ikiambatana na mafunzo urushaji ndege zisizo na rubani (drones), sambamba na maenesho ya bidhaa za kibunifu zilizoanza tarehe 19 – 21 Aprili 2023 na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 103 toka sekta mbalimbali zinazoendelea kufanyika kupitia Ukumbi wa Mikutano wa COSTECH uliopo Sayansi (Kijitonyama) – Jijini Dar es salaam.

Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu yanaendelea kufanyika nchi nzima na kilele chake kitadumu kwa siku tano (5) kuanzia tarehe 24 – 28 Aprili 2023 ikibeba kauli mbiu isemayo ” Ubunifu kwa Uchumi Shindani ” katika Uwanja wa Jamhuri – Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yanatumika kama chachu ya kwenda na mabadiliko na kasi ya Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Shindani ili kuhamasisha wabunifu wa ndani kuendelea kuchangamkia fursa zinazojitokeza na kuzidi kujipambanunua vyema katika maeneo yanayoleta tija kwa jamii ili kuunga mkono adhima ya Serikali ya kujenga mfumo thabiti wa Ubunifu Kitaifa.







No comments