Breaking News

ACT YATOA MAPENDEKEZO 15 RIPOTI YA CAG 2023

Chama cha ACT Wazalendo kimetoa mapendekezo 15 kufatia ripoti iliyosomwa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali 2023 (CAG) na kukabidhiwa kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. Samia Hassan kubaini kuwepo na ubadhilifu mkuwa wa mali ya umma.

Akizungumza wakati akiwasilisha uchambuzi uliofanywa na chama hicho 10 april jijini Dar es salaam kiongozi mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe amesema chama kimepitia na luichambua ripoti hiyo kama ambavyo wamekuwa wakifanya kila mwaka na kuja na mapendekezo haya 15.

Alisema kutokana na ripoti hiyo kuonyesha ubadhirifu mkubwa na baadhi ya watuhumiwa waliotajwa kuwa katika nafasi nyeti chama kimetoa ushauri na mapendekezo kwa serikali kama ifatavyo.

- Tunamsihi Rais Samia Suluhu Hassan akubali na kutekeleza pendekezo la CAG la kuunda Tume Huru ya Uchunguzi (Judicial Commission of Inquiry) kuhusu  ukiukwaji wa Maadili, Matumizi mabaya ya Ofisi na uporaji wa Mali za Watu uliofanywa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na sasa Jaji wa Mahakama Kuu Bwana Biswalo Mganga 

Hoja za Ukaguzi Mwaka wa Fedha 2021/2022

1. Hatari ya Mfuko wa Bima ya Afya
 
- Bodi na Menejimenti ya NHIF zibadilishwe 
- Mfumo wa Bima ya Afya na ule wa Hifadhi ya Jamii vifungamanishwe.
 
2. Deni la Taifa
- Tunaitaka Serikali kuheshimu Bunge na kufuata sheria ya Bajeti.
 
3. Upotevu usiokwisha wa Mabilioni ya Fedha za Mikopo kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu zinazotolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa .
- Tunapendekeza kuwa Mikopo kwa Vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu itolewe kupitia Skimu ya Hifadhi ya Jamii 

4. TANROAD haikujenga barabara mpya hata moja 2021/2022.
- Tunapendekeza kuwa Mheshimiwa Makame Mbarawa ajiuzulu na kuliomba radhi Bunge. 
- Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS ajiuzulu nafasi yake au Rais amfukuze kazi mara moja kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.
 
5. ATCL kukodisha ndege  kutoka TGFA
- Tunapendekeza ATCL imilikishwe ndege zote inazo kodishiwa kutoka TGFA.

6. Kuhusu Vishikwambi vya Sensa ya Watu na Makazi
- Tunapendekeza TAKUKURU kwa kushirikiana na Polisi wafanye uchunguzi wa kijinai katika mchakato mzima wa manunuzi ya vishikwambi vya sensa na wakati uchunguzi huo unaendelea watu wote waliohusika na mchakato wa manunuzi hayo wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi.
 
7. Mapungufu Mradi wa Mwendokasi na Matumizi ya Gesi Asilia badala ya Mafuta ya Dizeli
- Tunaitaka DART kuingia mkataba mara moja na TPDC kubadilisha mabasi ya mwendokasi kutoka kutumia Dizeli na kutumia gesi asilia (CNG).
- Mhandisi Mshauri wa Mradi afukuzwe kazi na kutafutwa mwengine mwenye uwezo 
 
8. Fedha Shilingi Bilioni 270 za CSR kwa Jamii zinazozunguka Mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere.
- Tunapendekeza kuwa  Mawaziri wa Nishati na TAMISEMI wasimamie na kuhakikisha makubaliano ya Mkataba yanatekelezwa kuanzia mwaka wa fedha unaoanza Julai 2023 ili wananchi wafaidike na Shilingi Bilioni 270 za CSR
 
9. Manunuzi katika mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati (SGR)
- Tunapendekeza  kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Kamati Teule ya Bunge kufanya uchunguzi wa kina.

10. Hoja za Ukaguzi TZS Bilioni 212 za UVIKO-19  
- Tunaitaka  Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote waliohusika katika ubadhirifu wa fedha hizi.

Hitimisho
- Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ina mtihani mmoja tu, nao ni kusafisha urathi (Legacy) wa maamuzi ya hovyo ya nyuma na kujenga Mfumo madhubuti wa kitaasisi ambao utazuia ubadhirifu wa Fedha za umma kwa faida kubwa ya uhai wa taifa, Tunamsihi Rais achukue hatua hizo.

 

No comments