Breaking News

JAMII YATAKIWA KUWAJENGEA MISINGI BORA WATOTO KATIKA LISHE ILI WAWEZE KUKUA KIAKILI

Mkurugenzi wa taasisi ya save of children bi Jane Mutua akiongea katika mkutano juu ya kukuza ufahamu wa kielimu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam
Head of Programs, Jamii Innitiative Godwin Mongi, akifafanua jambo katika mkutano huo

Dar es salaam:

Jamii imetakiwa kuwajengea misingi iliyobora ya kielimu kwa watoto ili kuweza kupata matokeo chanya kwa taifa na kwa vizazi vijavyo .

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa taasisi ya policy forum jijini Dar es saalam juu ya kukuza ufahamu wa kielimu kwa watoto mkurugenzi wa taasisi ya save of children bi Jane Mutua amesema kuwa pamoja na wazazi kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu ikiwemo chakula na malazi ni lazima jamii ijenge misingi bora ya kielimu kwa watoto wao ili kuweza kupata matokeo chanya kwa jamii yatakayoleta tija katika ngazi ya familia na kitaifa.

‘’katika utafiti huu tuliofanya katika wilaya Songwe tulifanya katika kubaini elimu ya awali ambapo tumebaini badhii ya wanafunzi hawana elimu ya awali hali inayopelekea uelewa mdogo kwa wanafunzi wa kieimu na ubunifu’’. Alisema Jane Mutua.

Alisema walimu wanao fundisha elimu ya awali ni lazima watumie mbinu wezeshi zitakazo wawezesha kukukuza uelewa na kujenga udadisi hali inapelekea watoto hao kuwa wabunifu na kuleta tija kwa taifa.

Alisema hatua za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa kuboresha hali ya ukuwaji wa mtoto kiakili ikiwa ni pamoja na kuwapa vyakula vyenye virutubishi ikiwemo samaki ni muhimu katika kukuza akili na uwezo wa mtoto hali inayopelekea mtoto huyo kuwa mbunifu .

‘’Ni mbinu gani tunazozitumia kwa watoto wetu ili kuweza kupata matokeo chanya kiakili na kuweza kuleta tija kwa taifa , wazazi wanalo jukumu la kuwalea watoto sio kimalezi tu bali hata vyakula vyenye virutubishi vitakavyo wajengea watoto kiakili’’. Aliongeza Jane Mutua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Bright Jamii Intiative, bwana Godwine Mungi amesema kuwa katika utafiti uliofanywa mwaka 2021 na taasisi hiyo ulibaini kuwa kumekuwa na uwekezaji mkubwa kwa vituo vya kuwalea watoto kielimu lakini kumekuwa na ombwe la taasisi hizo kuwekeza afya na lishe hali inayopelekea watoto hao kutofanya vizuri wawapo Darasani.

Alisema lazima taasisi zihamasishwe kuchangia watoto ilikuweza kuboresha mazingira ya kielimu ikiwemo utoaji wa chakula bora kitakacho wakuza watoto hao kiakili.



 

 

 

 


No comments