Breaking News

CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI UWEZI KUTENGANISHA

Na Heri Shaaban (Ilala)
CHAMA cha Mapinduzi CCM kimesema uwezi kutenganisha CCM na Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani CCM ndio inaunda Serikali kwa ajili ya kuongoza Dola.

Hayo yalisemwa na Mwenezi wa CCM kata ya Vingunguti  Mohamedi Muya, wakati wa Mkutano wa kata ya VINGUNGUTI Halmashauri ya Jiji kuhamasisha sensa ya Watu na Makazi kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa .

"Chama cha Mapinduzi CCM ndio kinaunda dola uwezi  KUTENGANISHA CCM na serikali  ya chama cha Mapinduzi ambacho kinasimamia Ilani ya Uchaguzi na popote kutakapokuwa na shughuli za Serikali CCM lazima inashiriki," alisema Mohamedi Muya .

Mwenezi Muya alisema Agosti 23 Mwaka huu ni siku ya kuhesabiwa ya sensa ya watu na makazi hivyo wananchi wote wa Vingunguti na Wilaya ya Ilala tuhesabiwe kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.

Kwa upande wake Meya wa Halmashauri  ya Jiji la Dar es Salaam, ambaye ni Diwani wa Vingunguti Omary Kumbilamoto, alisema Sensa ina faida nyingi ikiwemo kujua idadi ya wananchi ili Serikali iweze kuleta maendeleo kwa haraka hivyo watu wote wahesabiwe Ili serikali iweze kupanga malengo yake .

Meya Kumbilamoto alisema dhumuni la sensa ya Watu na Makazi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan iweze kujua idadi ya Watanzania na Wananchi wa Vingunguti hivyo kuhesabiwa ni haki yako ya Msingi usipoteze haki yako ya msingi.

"Serikali inapopanga bajeti yake sekta ya Elimu inatakiwa ijue Wananchi wangapi iweze kuongeza madarasa na Huduma za Jamii zikiwemo maji Barabara hivyo Wananchi wote muhesabiwe taarifa utazotoa ni za Siri wewe na karani wa sensa naomba muwape ushirikiano " alisema Kumbilamoto

Aliwataka viongozi wa dini vyama vya Siasa  kuhamasisha sensa ya Watu na Makazi mashabiki wao wahesabiwe .

Katibu wa CCM Vingunguti Agata Limbumba alisema  kwa niaba ya CCM anaungana na Serikali Kata ya VINGUNGUTI yote kuhamasisha sensa ya Watu na Makazi kwa manufaa ya Taifa usidanganyike kuhesabiwa ni haki ya Msingi kwa kila mtanzania.

Mwenyekiti wa Mtaa Mtakuja Sharifu Mburu alisema kwa niaba ya Kata ya VINGUNGUTI Wenyeviti wa Serikali za Mtaa wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awali tumeshiriki kuweka vibao vya anuani ya Makazi kwa sasa tumepata anuani za makazi mitaa yetu inatambulika kituo kinachofuta sensa kuhesabiwa Watanzania wote

No comments