Breaking News

WAZIRI NDUMBALO : SERIKALI ITAENDELEA KUSHIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA WANYAMAPORI NCHINI

Na : Timothy Marko
Serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya wanyamapori hili kuweza kujadili juu ya zuio liliotolewa mei 25 Mwaka huu la usafirishaji wa wanyapori na maliasili nchini Kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na tija hapa nchini.

Akizungumza na wadau wa Biashara ya  wa wanyamapori hai  jijini Dar es Salaam Waziri wa Maliasili na utalii, Mhe Damas Ndumbalo amesema Serikali inaendelea kuitambua sekta hiyo pamoja na wadau wake katika kukuza Uchumi wa  nchi.

"Waziri mkuu anafahamu sakata hili la  zuio la usafirishaji wanyamapori hai liliotolewa aliyekuwa Waziri maliasili na utalii Profesa Jumanne magembe". Alisema Waziri Ndumbalo.

Alisema Serikali ipo katika mchakato wa kulitafutia majawabu sakata Hilo hivyo wadau  wa sekta hiyo wawe na uvumilivu.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha wasafirisha viumbe hai nchini(TWEA) Abraham Warioba alisema walitarajia Serikali kuondoa zui Hilo kwani kinachofanyika hivi sasa wanaweka wanyamapori kwenye zizi jambo ambalo ni hatari.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanachama cha wasafirishaji wanyamapori nchini Enock Balilemwa alisema kumekuwepo na kauli za Baadhi ya viongozi wa kiserikal kutowasaidia bali wanataka  hivyo kutafuta uvumbuzi wa kero zaa wadau wa sekta hiyo.

 

No comments