Breaking News

KIMOMWE MOTORS YAMTANGAZA MCHEKESHAJI MKOJANI BALOZI WA KAMPUNI YAO

Kampuni ya ya uagizaji wa magari kutoka nje ya nchi Kimomwe Motors ya jijini Dar es salaam leo imemtambulisha rasmi mchekeshaji maarufu hapa nchini anayejulikana kama Mkojani kama balozi wa Kampuni hiyo.

Akizungumza katika hafla fupi ya kumtambulisha Mkojani kama balozi wa kampuni hiyo mwanzilishi wa Kimwomwe Motors, bw. Selemani kimomwe amesema wameamua kumtumia msanii huyo kama balozi wa kampuni hiyo kutokana na kufanya kwake vizuri katika sanaa hapa nchini huku wakiamini kuwa atakuwa balozi ambaye ataiwakilisha vyema kampuni kwa wateja wake.

"Kampuni yetu kwa sasa ina miaka mitatu tangu tuianzishe mwaka 2018 na imekuwa ikifanya vizuri siku baada ya siku kwani wateja wengi wameendelea kutuamini kama sehemu yao ya uagizaji wa magari kutoka nchi za Japan, Singapore na Uk hivyo leo tumemtambulisha mkojani kama balozi wetu kuyaendeleza mazuri yanayopatikana ndani ya kampuni ya Kimomwe Motors" alisema bw. Kimomwe

Ameongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha mteja atakayeagiza gari yake kupitia Kimomwe Motors anafikishiwa gari yake ndani ya siku 45 ambapo asilimia 50 ya thamani ya gari atailipa kabla ya gari yake kufika nchini na kiasi kilichobaki kitalipwa baada ya gari kufika na kuongeza kuwa endapo mteja aliyeagiza gari yake atashindwa kumalizia kiasi kilichobaki baada ya gari yake kufikishwa nchini kampuni hiyo itamuunganisha na taasisi ya mikopo ili kuona ni jinsi gani mteja atamalizia fedha hizo.

Hata hivyo katika hatua nyingine kampuni hiyo imemkabidhi msanii huyo gari jipya aina ya BMW kulitumia kwa muda kabla ya kumpatia zawadi nyingine kubwa mwezi desember mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari hilo na kutambulishwa kama balozi wa kampuni ya Kimomwe Motors, Abdallah Mohamed Nzunda maarufu kama Mkojani ameishukuru kampuni hiyo kwa kumchagua kama balozi wake licha ya kuwepo kwa wasanii wengi wanaofanya vizuri nchini na kuahidi kuwa ataitumia fursa hiyo pia kutoa elimu kwa watanzania juu ya namna ya kuagiza gari nje ya nchi kupitia kampuni ya Kimomwe 

"Nitoe shukrani za dhati kwa kampuni ya Kimomwe kwa kuona kipaji changu, niwahakikishie kuwa nitafanya kazi kwa kiwango cha hali ya juu kwa ukizingatia kampuni tayali inafanya kazi katika viwango vya kimataifa hivyo sitawaangusha" Alisema Mkojan.

No comments