Breaking News

TIC, ZIPA Zatiliana Saini Ushirikiano Maeneo 12 Kukuza Sekta Ya Uwekezaji

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Dr. Maduhu Kazi (kushoto) kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukuzaji Uwekezaji Zanzibarm (ZIPA) Shariff Shariff wakisaini Makubaliano ushirikiano kukuza sekta ya uwekezaji Tanzania bara na Zanzibar.
Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) kimetiliana saini ya mashirikiano na Mamlaka ya Ukuzaji Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa ajili ya kutekeleza maeneo kumi na mbili muhimu katika sekta ya uwekezaji.

Akizungumza baada ya kutiliana saini Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dr. Maduhu Kazi alisema lengo kubwa la makubaliano hayo ni kukuza sekta ya uwekezaji upande wa Tanzania bara na Zanzibar.

Alisema katika mashirikiano hayo yapo maeneo ambayo yamepewa msukumo kubwa kama kufanya tafiti za vyanzo vya uwekezaji, kubadilishana taarifa na uzoefu na ujuzi kwa wafanyakazi wa taasisi hizo.

"Kupitia mashirikiano haya tutashirikiana na ZIPA kutangaza vivutio vyetu vya uwekezaji, kuandaa maonyesho ya uwekezaji, kujitangaza na kuvutia wawekezaji, pamoja na kubadilishana uzoefu na ujuzi kwa watumishi wetu" Alisema Dr Kazi

Dr. Kazi aliongeza kuwa masuala ya kimfumo (Tehama) kuhusisha pande zote mbili (Tanzania Bara na Zanzibar) tayari wataalamu wameanza kuyafanyia kazi.

"Ripoti zinaonyesha kuwa hali ya uwekezaji nchini inazidi kuimalika licha ya kuwepo kwa ujanga la UVICO 19, hivyo mashirikiano haya yataongeza zaidi idadi ya wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ukuzaji Uwekezaji Zanzibar, (ZIPA)Bw. Shariff Shariff alisema mashirikiano hayo yatasaidia kupiga hatua kubwa katika kutangaza vivutio vya uwekezaji ili kukuza sekta hiyo.

"Mashirikiano kati ya ZIPA na TIC yatasaidia kuongeza mafanikio, hivyo  tutahakikisha tunafanya kazi hizi kwa pamoja ili kufikia malengo yetu" Alisema bw. Shariff.
Alisema mashirikiano tayali yamebarikiwa na wakuu wa nchi, hivyo tutashirikiana vizuri kutekeleza mambo muhimu kukuza sekta ya uwekezaji na kutangaza vivutio vya uwekezaji vya Tanzania bara na Visiwani Zanzibar.

No comments