WFC Yapunguza Kiwango Cha TOZO kwa Waajiri Sekta Binafsi
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Mkurugenzi Mtendaji wa WCF, Dkt. John Mduma akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari ofisi za WCF, Jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umetangaza rasmi kupunguza kiwango cha tozo kwa waajiri wa sekta binafsi kutoka asilimia moja hadi 0.6 kuanzia michango ya Julai mwaka huu, ikiwa ni punguzo la asilimia 40, ili kuboresha mazingira ya biashara.
Akizungumza kuhusu kushuka kwa tozo hizo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa WCF, Dkt. John Mduma, alisema marekebisho hayo yanafuatia uamuzi wa Bunge ambalo lilipitisha kiwango hicho cha tozo kwa sekta binafsi.
“Dhamira ya hatua hii ni kuzifanya sekta binafsi kutumia masalio ya fedha hizo katika uzalishaji, hivyo tumewapunguzia mzigo ili kukuza biashara zao”. Alisema Dkt.Mduma.
Alisema hatua hiyo inaboresha mazingira ya biashara nchini kama inavyoelekeza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu kuziboresha taasisi kwa kuzipunguzia tozo.
"Hatua hii imelenga kuleta mahusiano mazuri kati ya mfuko huo na waajiri, hatimaye kuchangia ukuaji uchumi"
Dokta Mduma aliongeza kuwa pamoja na kupunguza kiwango cha michango kwa sekta binafsi, lakini mafao yanabaki kama yalivyokuwa awali.
Alisema mpaka kukamilika Mchakato huo umepitia hatua mbalimbali hivyo kuchukua fursa hiyo kushukuru Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ambao wote kwa pamoja tumeshirikiana kufikia hatua hii.
Dkt. Mduma aliongeza kuwa kwa sasa mfuko huo una thamani ya sh. bilioni 437 na kwamba kumekuwa na kasi kubwa ya ongezeko la wachangiaji.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar akitoa ufafanuzia kwa waandishi wa habari katika ofisi za WCF Jijini Dar es Salaam.
Nae Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, alisema mfuko una jumla ya wachangiaji 24,952 na kati yao sekta binafsi ni asilimia 70 huku 30 ni sekta ya umma.
Aliongeza pamoja na kupunguza asilimia ya michango, lakini tathmini zinaonyesha WCF itakuwa na afya kwa zaidi ya miaka 30 kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Alisema hadi sasa tayari wameshabadilisha mifumo yao ya kielektroniki, hivyo yeyote atakayelipa atatumia kikokotoo kipya cha asilimia 0.6.
Kuhusu idadi ya wachangiaji wanaozingatia michango hiyo, Peter amesema ni asilimia 82 huku waliobaki ndiyo changamoto.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema kuwa kiwango cha michango kwa sekta ya umma ni asilimia 0.5 huku sekta binafsi ni asilimia 0.6.
Alisema sababu za tofauti ya michango hiyo ni hali hatarishi zaidi kwa wafanyakazi wa sekta binafsi ukilinganisha na sekta ya umma kutokana na shughuli zao.
No comments