Breaking News

Uingizwaji wa Dawa za Kulevya Wapungua 95% Nchini

Kiwango cha uingizaji Madawa ya Kulevya nchini kimepungua kwa asilimia 95 huku  kuwa changamoto iliyopo sasa ni kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya aina ya Bangi hapa.

Katibu MKuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe.Tixon Nzunda, amebainisha hayo wakati akizingumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya kutembelea Makao makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini (DCEA) Jijini  Dar es Salaam kwa lengo la kujionea inavyofanya kazi.

"Kwa sasa matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi yameongezeka nchini tofauti na miaka ya nyuma huivyo natoa wito kwa Viongozi wa Dini na mashirika mbali mbali kuungana katika kupambana kwenye vita ya matumizi ya Bangi kwani yanaathari kubwa". Amesema Mhe.Nzunda.
 
Mhe. Nzunda pia amewatadhalisha wafanyabiashara wa Madawa ya Kulevya pamoja watumiaji na kudai kuwa Tanzania sio sehemu salama kwao kutokana na mikakati iliyowekwa na Mamlaka hiyo katika kupambana na madawa ya kulevya.

alisema serikali ya awamu ya sita itaendelea kutoa nguvu kubwa kwenye Mamlaka hiyo ili kuzidisha vita ya kupambana na madawa ya kulevya nchini

Kwa upande wake Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya chini, Gerald Kusaya amewaonya wale ambao bado wanajihusisha na biashara na usafirishaji wa madawa ya kulevya kuacha mara moja hivyo mamlaka hiyo itaendelea kuwatafuta kwa kushirikiana na jeshi la  polisi pamoja na wananchi


No comments