Bi Sofia: Jamii Bado Ina Uelewa Mdogo Juu ya Haki za Wanawake na Watoto
KITUO cha kupinga ukatili wa kijinsia (CAGBV) Dar es Salaam kimesema kitaendelea na programu ya utoaji wa elimu ya sheria za mirathi kwa makundi mbalimbali ya akinamama ili kuiwezesha jamii hiyo kufahamu haki zao baada ya kuondokewa na wapendwa wao.
Alisema familia nyingi hudiriki kuwanyanyapaa wanawake ama watoto kwa lengo la kujimilikisha mali zilizoachwa na marehemu.
Akizungumza Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Sofia Komba amesema kumekuwa na changamoto mbalimbali za kupokonywa mali katika baadhi ya familia mara wanapoondokewa na mpendwa wao kwakutozifahamu sheria za mirathi.
"Programu hizi za mafunzo tunazoziendesha huyasaidia makundi ya akinamama na watoto kutambua haki za msingi katika familia mara baada ya waume wao kuaga dunia," amesema Bi Sofia
Bi Sofia ameeleza kwamba ndugu na jamaa wa karibu hujitokeza kwa minajili ya kuchukua mali ama nyaraka muhimu ili kunufaika nazo ambapo kama taasisi huwakusanya akinamama kwa lengo la kuwajengea uwezo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo amesema pia hujishughulisha na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wanaoelekea ukubwani ili kujiepusha na mimba za utotoni sambamba na magonjwa ya zinaa yatokanayo na mahusiano.
Hata hivyo kutokana na wimbi la matukio yasiopendeza yatokanayo na huduma za afya taasisi imeishauri serikali kuboresha miundombinu kwa weredi ili kuweza kupunguza vifo vya watoto na akinamama.
No comments