Breaking News

Jesho la Zimamoto Yakusanya Zaidi bilioni 1 Mwaka 2020/21

JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala Dar es Salaam limepata mafanikio makubwa katika mwaka wa Serikali 2020/2021 kwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1 na milion 302 cha mapato ya kodi na kuzidi kiwango cha makadirio ya shilingi bilioni 1 na milioni 250 kilichopangwa na Serikali.

Akitoa taarifa hiyo Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari Mratibu Msaidizi Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ilala Elisa Mugisha alisema mafanikio hayo yametokana na wadau kujitokeza kwa kulipa tozo zao bila usumbufu.

"Tumefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni 302 kwa kuvuka kiwango kilichopangwa na Serikali hiyo imetokana na ushiriki wa wadau wetu kuweza kutimiza wajibu wa kulipa tozo za huduma mbalimbali  kupitia jeshi la zimamoto na Uokoaji," alisema Kamanda Mugisha.

Aidha Kamanda Mugisha alisema kwamba kikosi cha zimamoto na uokoaji wamekuwa wakitoa huduma kwa jamii kuepukana na vihatarishi vilivyoko katika makazi yao kwa kuona shughuli zinafanyika katika hali ya usalama na kudai kuwawajibu wao sio kufungia huduma zitolewazo kwa wananchi.

Kikosi hicho mbali na kutekeleza majukumu yake ya Zimamoto na uokoaji limekabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kupata taarifa ambazo sio sahihi hata hivyo limewataka wateja wengine ambao hawakupata fursa ya kulipia huduma hizo wafanye jitihada za kukamilisha malipo hayo.

Kamanda huyo alisema wamekuwa wakipokea taarifa mbalimbali za milipuko ya moto inayotokana na vihatarishi kutoka kwa wananchi na kudai kuboresha huduma hizo kwa weredi na kufika kwenye matukio kwa wakati.

Wito umetolewa kwa wadau wa mkoa wa Ilala kufika ofisi za jeshi hilo kwa lengo la kupatiwa elimu zaidi kuhusiana na taratibu zinazoratibiwa jeshi hilo kupitia huduma za msingi katika kujiepusha na vihatarishi vinavyosababisha majanga ya moto.
 

No comments