Indonesia Kivutio Maonyesho ya Vyakula Asili Jijini Dar
MAONYESHO ya kimataifa ya vyakula vya kitamaduni kutoka nchi mbalimbali Duniani yamehudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kushuhudia namna ya uandaaji wake pamoja na kupata radha ya vyakula hivyo.
Amesema nchi Indonesia hutumia viungo mbalimbali katika uandaaji wa vyakula hivyo ambapo pia hupatikana katika nchi ya Tanzania ikiwemo mihogo,ndizi, viazi mviringo na karanga.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya vyakula hivyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Balozi kutoka Ubalozi wa Indonesia nchini Wahono Yulianto amesema maonyesho hayo yanawapa fursa watanzania kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka nchi nyingine.
"Lengo la maonyesho haya ni kujenga mahusiano pamoja na kuwaonyesha watanzania aina mbalimbali ya vyakula vinavyopatikana nchini Indonesia kiasi ambacho hupikwa kwa kutumia viungo ambavyo pia hupatikana Tanzania," amesema Yulianto
Aidha Kaimu huyo amesema kwa kuongeza kwamba maonyesho hayo yanaweza kutumika kama njia ya kufahamiana kwa kujenga mahusiano mema baina ya nchi Indonesia na Tanzania sambamba na taasisi zingine zilizoshiriki maonyesho hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Indonesia Joan Radina Setiawan alieleza ushiriki wao kwenye maonyesho ni pamoja na utoji wa mafunzo ya mapishi kwa makundi mbalimbali ya wanajamii kwa kudai kwamba ni sehemu ya utamaduni katika nchi yao.
Hata hivyo Mkuu huyo alifafanua kuwa upikaji wa chakula kizuri unatokana na ubunifu aliokuwa nao muandaaji ambaye hutumia maarifa kwa kukifanya kinakuwa na radha bora yenye kumvutia mlaji.
Nae muandaaji wa Maonyesho kutoka taasisi ya Sapota hapa nchini Ally Mchume amesema maonyesho hayo alikuwa ya siku 3 yamezishirikisha zaidi ya nchi 15 Duniani zikiwemo China,Tanzania,Indonesia, Mexico,Vietnam na Ufaransa.
"Maonyesho haya yanalengo la kujenga mahusiano mema ya kitamaduni kati ya nchi hizi ambapo Tanzania kama mwenyeji imeonesha umadhubuti katika uandaaji wa vyakula bora vya kitamaduni," alisema Mchume.
No comments