Waitara Aitaka TPA Kuendelea Kutoa Huduma Bora Zaidi
SERIKALI imesema jicho lake liko kwenye Bandari ya Dar es Salaam, kwa kuwa ni eneo muhimu katika maendeleo ya uchumi wa nchi na ni lango kuu la kibiashara.
Alisema sehemu kubwa ya mapato ya nchi yanapatikana kupitia bandari hiyo, hivyo serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haitaki masihara na yeyote atakae thubutu kuleta mzaha.
Akizungumza jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara mara alipofanya ziara kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Dar es Salaam na kuzungumza na menejimenti ya Mamlaka hiyo na Bandari.
Katika ziara hiyo ambayo alihimiza huduma nzuri kwa wateja na kukemea uwepo wa makundi miongoni mwa wafanyakazi katika bandari hiyo na kudai yanaweza kuathiri ufanisi wa utoaji huduma.
"Wateja wanapohudumiwa vizuri wanakuwa mabalozi wa kupeleka ujumbe mzuri kwenye nchi jirani kwa kuwambia wengine kuwa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ipo vizuri," alisema Waitara
Katika ziara hiyo Waitara aliwataka wafanyakazi wote wa TPA kuanzia uongozi wa juu mpaka langoni kutambua kwamba Serikali pamoja na wananchi wanawategemea katika utendaji wa majukumu yao.
Alisema wanapotoa huduma wajue wanatoa huduma kwa niaba ya watanzania wengi wanaotazama kazi yako waone ni nzuri. Rais Samia anaposema tunataka fedha safi na kodi ambayo siyo ya kushurutisha na kufilisi watu anamaanisha watu ambao mmesimama mahali ambapo kuna biashara, ifanyike biashara halali.
Hivyo Naibu Waziri alikemea uwepo wa makundi miongoni mwa wafanyakazi na kudai anataarifa za uwepo wa kundi linalojiita wenyeji wenye bandari yao na kundi linaloitwa wakuja, ambapo alisema wanaotumia kauli hiyo Serikali haitaki kuzisikia.
Katika hatua nyingine Waitara aliitaka TPA kushughulikia matatizo ya tozo za nauli katika kivuko cha Buchosa kilichopo Mkoani Mwanza na Nyamisati kilichopo Mafia ambakp wananchi wanalipa kiasi cha sh.1200 kitu ambacho Rais Samia alishaagiza kifanyiwe kazi.
No comments