LHRC Yalaani Mauaji ya kikatili ya Mtoto Mkoani Tabora
KITUO cha sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimelaani mauaji ya kikatili ya mtoto Nyanzobhe Mwandu mwenye umri wa miaka minne yaliyotokea juni 16 Mkoani Tabora baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuchomwa na watu waliosadikiwa kuwa ni askari wa wa hifashi ya wanyama pori nchini TAWA wakishirikiana na askari polisi wa kituo cha Igagala namba 5.
Mauaji hayo yametelezwa baada ya aliyekuwa mkuu wa wilaya Kaliua akitoa maagizo ya kuchoma nyumba za wanakijiji ambao wanazunguka hifadhi ya kijiji ya Ngitiri.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Bi Anna Henga alisema kuwa mauaji hayo ni kinyama yanafaa kulaaniwa kwa nguvu zote na kwamba aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kaliua Abel Busalama yeji yakuwa anawajibika dhidi ya kitendo hicho.
"Kituo cha sheria na haki za Binadamu kinalaani kitendo hicho na kutaka wahusika wa mauaji hayo kuchukuliwa hatua za kisheria kufuatia ukiukwaji wa katiba ya nchi na pia haki za binadamu ambapo ndugu wahabari ibara ya 24 (1) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho inasema kila mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria," alisema Bi Anna
Na kuongeza kuwa ibara ya 14 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake inatamka wazi kwamba kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria.
Aidha ameiomba wizara ya TAMISEMI ihakikishe mipaka yote ya vijiji vinavyopakana na ardhi ya hifadhi inawekwa bayana ili wananchi wafahamu mipaka ya vijiji vyao ilipoishia pamoja na kuhakikisha vijiji visivyo athirika na amri ya mkuu wa wilaya vinabaki salama na wananchi waruhusiwe kuanza kuvuna mazao yao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Uchechemuzi wa Maboresho LHRC Joseph Oleshangay alisema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya kikatili na kuitaka serikali iendelee kuchukua hatua ili kukomesha vitendo hivyo vya kikatili vinavyofanwa na baadhi ya watu.
"Kuna matukio mengi ya kikatili yanayofanywa na baadhi ya watu hivyo tunaitaka serikali na Mamlaka zingine ziendelee kuchukua hatua ili kukomesha matukio hayo," alisema Oleshangay.
No comments