Majaliwa: Awataka Watafiti na Wabunifu Kuongeza Kasi ya Kufanya Tafiti Nchi iende sambamba na mabadiliko Yanayotokea Ulimwenguni
WAZIRI MKuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim majaliwa ametoa maelekezo kwa vyuo vyote nchini kuweka utaratibu wa kufanya tafiti kwa kuonyesha matokeo itapelekea kukua kwa sekta ya ajira.
Pia amevitaka viwanda kuunga mkono tafiti mbalimbali kwa kuongeza bajeti ili kuwawezesha wanaofanya tafiti .
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa maadhimosho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu alisema vyuo vyote viwe na utaratibu kama chuo kikuu cha Dar es Salaam chakufanya tafiti mbalimbali.
Majaliwa alisema chuo kikuu cha Dar es Salaam kinafanya kazi nzuri kwa kuendesha tafiti,mbalimbali, lakini ziangaliwe tafiti zinazofanywa zinatatua changamoto zilizopo katika jamii.
Aidha alisema amefarijika kwa kuona tafiti zinazofanywa na chuo cha Dar es Salaam kwa kutoa kipaumbele kufanya tafiti.
Alitoa wito kwa chuo hicho kuendelea kufanya tafiti mbalimbali na wasizifungie kwenye makabati.
Alisema kuna umuhimu wa tafiti katika kuhakikisha wanaendana na mabadiliko hayo hawana budi kutilia mkazo tafiti hizo.
Alisema kupitia tafiti hizo kuna ibua changamoto katika maeneo ya kufanyia kazi, hivyo Serikali imeahidi kuendelea kutenga baajeti za kuendeshea tafiti hizo.
"Serikali imeona kuna umuhimu wa kuongeza bajeti, wasomi waweze kunufaika na tafiti wanazofanya" Alisema
Pia alitoa wito kwa viwanda na wafanyabiashara pamoja na wachumi kuunganisha tafiti ili kuleta tija.
Aliongeza hivi karibuni alipokuwa jijini Dodoma aligundua kuna udhaifu kidogo hivyo amewahakikishia kufanya maboresho.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako alisema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa mbalimbali ambapo malengo ya Serikali inatoa kipaumbele katika utafiti mwaka 2021 hadi 2022 .
Hatahivyo alisema wizara itaendelea kuimarisha sayansi na ubunifu ambao utaendelea kupewa kipaumbele ili kuongeza teknolojia.
No comments