Dk.Mlyuka: Jamii Bado Aina Mwamko Juu Ya Matumizi ya Nishati Mbadala
WABUNIFU na watafiti wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametengeneza majiko yanayotumia nguvu ya jua ikiwa lengo ni kupunguza gharama za maisha kwa watumiaji juu ya matumizi ya nishati nyingine.
Akizungumza katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya sita ya utafiti na ubunifu Mhadhili Idara ya Fizikia, Ndaki ya Sayansi Asilia na tumizi, Dk. Nuru Mlyuka alisema kuwa matumizi ya nishati hiyo, bado muamko ni mdogo hasa kwa maeneo ya vijijini.
Dk.Mlyuka alisema kuwa pamoja na kuwepo na jitihada za makusudi na tafiti mbalimbali juu ya matumizi ya nishati mbadala bado kumekuwepo na mwitiko mdogo kwa jamii hapa nchini.
Aidha alisema pamoja na changamoto hizo , watafiti wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali kwa lengo kuiwezesha jamii kupata tekinolojia ambayo itaweza kukidhi matumizi yao.
Alisema jiko hilo ambalo limebuniwa mahususi kwa lengo la kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuongeza wigo kwa wananchi kuachana na matumizi ya mkaa.
"Lengo la mradi huu wa jiko la nguvu za jua ni kuongeza kasi ya kupunguza matumizi ya nishati ya mkaa na kuni na kupunguza ukataji miti na kupunguza gharama kwakuwa jiko hilo linatumia jua kupika" alisema.
Alifafanua kuwa hakuna teknolojia isiyokuwa na changamoto kwasababu jiko hilo linatakiwa lipikiwe nje ambapo ni changamoto ndogo ikilinganishwa na matumizi ya kuni.
Post Comment
No comments