Breaking News

Vijana NCCR Mageuzi Waitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini Kutokiuka Makubaliano Yake na Wanafunzi


TAARIFA YA KITENGO CHA VIJANA NCCR MAGEUZI KUHUSU UPATIKANAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Kwanza tunatoa salamu za rambirambi kwa Watanzania wote pamoja na familia ya Rais wa awamu ya tatu Ndugu Benjamin William Mkapa. Pia tunaungana na familia na Watanzania wote kuomboleza msiba huu mzito wa Taifa.

MIKOPO VYUO VIKUU
Ndugu waandishi wa habari, Kama mnavyofahamu  bodi ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu imetoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini. 

Tumeshangazwa na taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi siku ya Jumatatu 20 Julai, 2020 ikisema “wanafunzi wote wanufaika wa mikopo watalipwa stahiki zao za robo ya nne kwa siku ambazo watakuwa vyuoni kwa siku za masomo” 

Changamoto iliyojitokeza katika mchakato huu fedha imepungua mbali na makubaliano kati ya Bodi na wanufaika (wanafunzi). Jambo hili sio la kawaida na limezua sintofahamu kwa wanufaika wa mikopo hiyo.

Ndugu wanahabari, tumeweza kufuatilia kwa ukaribu zaidi na kuabini changamoto kadhaa za kisheria na kimiongozo ambayo inaongoza Bodi na Utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi.

Miezi mitatu kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha, mkurugenzi wa  bodi ya mikopo hutakiwa kuandaa makadilio ya mapato na matumizi ya bodi kwa mwaka husika na makadirio hayo huusisha (Ada, Viandikwa, Utafiti, Mafunzo kwa Vitendo, Kujikimu na Malazi, Mahitaji maalum) mchakato ambao ulishafanywa na kiasi kilitengwa kwa kila mnufaika kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Mnamo 21 Mei 2020, Bodi ya mikopo ilitoa ufafanuzi kuwa malipo yote kwa wanufaika yatafanyika kama hapo awali na fedha za wanufaika zipo na tayari wameshaanza mchakato wa kuzifikisha kwa walengwa.

Suala la mikopo kati ya Bodi na wanufaika (Wanafunzi) ni suala la kimkataba na linalindwa na sharia za kimkataba, hivyo uamuzi wa kutoa fedha kulingana na siku ambazo wanufaikia (wanafunzi) wako vyuoni ni ukiukwaji wa shera za kimkataba. 

Kwani fedha hizo ni mkopo halali na wanufaika watapaswa kuzirudisha baada ya kumaliza masomo hivyo hakukuwa na sababu yeyote ya kupunguza fedha kwa kutumia kigezo cha siku kupungua. 

Mkopo ni haki ya mnufaika na tayari fedha zilishapangwa kutolewa na bodi ya mikopo yenyewe kama ilivyosema 21 Mei 2020.

Mabadiliko ya kimfumo na kimaisha yaliyochangiwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID19) na Uamuzi wa Bodi ya mikopo kuamua kutoa fedha ya kujikimu pungufu kulingana na siku zilizobaki bilamkuta taarifa si uungwana. 

Hii ni kwa sasa mahitaji ya wanfunzi yameongezeka na gharama za maisha pia zimeongezeka, mahitaji ya vitakasa mikono, barakoa, na usomaji wa mitandaoni. 

Bodi ilipaswa kuliangalia hili jambo kw aumakini zaidi na kuwapatia wanafunzi fedha zao zote iliwaweze kuendana na mabadiliko yaliyopo.

Ndugu waandishi wa habari, kwa mujibu wa sheria na miongozo mbalimbali ya bodi ya mikopo, hakuna mahali popote ambapo bodi inayomamlaka ya kupunguza au kuongeza kiwango chhochote cha fedha anayopangiwa mnufaika wa mikopo isipokuwa kwa utaratibu maalum wa Rufaa nk.

 Mfano; muongozo wa bodi ya mikopo 2018/2019 kipengele No.3 kinaeleza “kusipokuwa na kuongezwa kipengele chochote mwaka husika, kiasi anachopangiwa mwanafunzi kitakuwa kilekile kwa miaka yake ya masomo” vile vile kipenge No. 5.4 kimeeleza “Wanafunzi wote wanufaika wanaoendelea na masomo wataendelea kupokea mikopo kama awali kulingana na ufaulu wa mitihani yao”

Ndugu waandishi wa habari, Tunaisisitizia Bodi ya Mikopo ifuate makubaliano ya kimkataba na wanufaika wa mikopo hiyo kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyowekwa ya utoaji wa mikopo hiyo. 

Pia tunawasisitizia Viongozi wa Serikali za wanafunzi kuchukua hatua ya kwenda mahakamani kufungua shauri la kutaka tafsiri na kushinikiza Bodi ya Mikopo kufuata Sheria na miongozo na makubaliano kati yao na wanufaika (wanafunzi)

USHIRIKI WA VIJANA UCHAGUZI MKUU 2020
Ndugu waandishi wa habari, Napenda nichukue nafasi hii kuwasisitizia wanachama wa NCCR-Mageuzi na Vijana kwa ujumla kujitokeza kuchukua fomu za nafasi mbalimbali za kiungozi kwenye uchaguzi mkuu 2020.

Hii ni fursa na nafasi kwetu sisi vijana kufanya mabadiliko na kuleta maendeleo chanya kwenye jamii na taifa letu kwa ujumla.

Imetolewa na;
Kitentya Luth
Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mawasiliano ya Umma
KITENGO cha Vijana NCCR-Mageuzi.

3 comments:

  1. Hiki chama kinakuja vizuri katika ujio wake wa pili. Kiliyumba mwaka 1998. Kinarejea mwaka huu

    ReplyDelete
  2. Hiki chama kinakuja vizuri katika ujio wake wa pili. Kiliyumba mwaka 1998. Kinarejea mwaka huu

    ReplyDelete
  3. Bodi imeegemea upande mmoja. Imeshindwa kutambua kuwa sio wanufaika wote wanalipiwa ada (school fee) na pesa ya kujikimu (boom).
    Bodi imeshindwa kutambua kuwa wapo wanufaika ambao hutegemea pesa ya kujikimu kulipa ada

    ReplyDelete