Breaking News

Mkutano Mkuu CUF Wampitisha Kwa Kishindo Profesa Lipumba Kuwa Mgombea Wa Urais CUF Tanzania Bara.. Juma Haji Kombo Kwa Upande Wa Zanzibar


Mkutano Mkuu huo maalum Umempitisha Mhe Prof Ibrahim Haruna Lipumba kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 97.2% ya wajumbe wote.

Aidha Mkutano Mkuu huo maalum umempitisha Mh Mussa Haji kombo kuwa mgombea Urais wa Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwa 66% ya kura zote zilizopigwa,huku  Eng: Mohamed Habib Mnyaa akipata 19% na mh Rajab Mbarouk Mohamed akipata 15%.

 Mkutano huo pia umempitisha Mhe. Hamida Huweish kwa asilimia 100% kuwa mgombea mwenza wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine mkutano  mkuu huo Maalum wa CUF - Chama cha Wananchi umemvua Umakamu Mwenyekiti Zanzibar Mhe Abbas Juma Muhunzi ambaye awali alisimamishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa lililoketi Juni 28 -30 mwaka huu. 

Kwa kuzingatia Ibara za 91(1), 91(2), 83 (3),  77 (7) (d)  , 103 na 97 za Katiba ya mwaka 1992 ya CUF- Chama cha Wananchi Toleo la 2019 wajumbe 537 kutoka Tanzania Bara walipiga kura ambapo wajumbe 531 walikubali Mhe. Muhunzi kuvuliwa Umakamu Mwenyekiti na wajumbe 6 walipinga Kwa upande wa wajumbe kutoka Zanzibar wajumbe 219 waliunga mkono kuondolewa kwa Mhe. Muhunzi kwenye nafasi hiyo na wajumbe 9 walikataa. 

Hivyo Mhe. 
Muhunzi amevuliwa Umakamu Mwenyekiti kwa zaidi ya theluthi mbili ya kura za wajumbe wa kila upande wa Muungano kama inavyotaka Katiba ya Chama katika Maamuzi Muhimu.

Kufuatia Maamuzi hayo, Mkutano Mkuu wa CUF-Chama cha Wananchi umemteua kwa kauli moja mhe. Mussa Haji Kombo kuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti Zanzibar kwa kuwa nafasi hiyo haiwezi kuzibwa kwa Uchaguzi mpaka zipite siku 180 tangu kuanzia leo. 

No comments