Rc MAKONDA Apokea Shehena ga Vifaa Vya Kujikinga na CORONA Kutoka Kwa ROSTAM AZIZI
Mfanyabiashara Maarufu Nchini Rostam Aziz chini ya Kampuni ya Taifa Gas leo amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Shehena ya Vifaa vya Kisasa vya Kuwakinga Wananchi dhidi ya virusi vya Corona vyenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 600.
Vifaa alivyopatiwa RC Makonda ni Mashine za kisasa 25 zenye uwezo wa kumtakasa mtu na kuua vijidudu mwili mzima, Barakoa 70,000, Dumu 600 za ujazo wa Lita 5 zenye Dawa ya kunawa mikono pamoja na Sanitizer 600.
RC Makonda amesema Mashine hizo 25 zitapelekwa kwenye maeneo yenye msongamano wa watu kama Vituo vya Daladala na Masokoni na Dawa za kunawia mikono zitagawanywa kwa Watu wa Daladala kwaajili ya kuhakikisha kila abiria ananawa mikono.
Aidha RC Makonda amemshukuru Mfanyabiashara Rostam Aziz kwa upendo na moyo wa kuwajali wananchi wa Dar es salaam ambapo amesema atahakikisha kila kifaa kinamfikia mlengwa.
Pamoja na hayo RC Makonda amewataka wananchi kuendelea kuchukuwa tahadhari dhidi ugonjwa wa Corona kwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya.
Kwa Upande wake Mfanyabiashara Rostam Aziz alisema ataendelea kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo katika mambo mbalimbali ya kijamii ambapo msaada aliotoa keo ni mwanzo tu wa ushirikiano.
No comments