Rais MAGUFULI Amefanya Uteuzi Huu Leo March 23.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi
wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Benjamin Mkapa, Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini
Mkapa, Dodoma.
Taarifa iliyotolewa leo March 23 , 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P.
Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)
kuanzia tarehe 22 March, 2018.
Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo
cha Elimu ya Biashara (CBE) kitivo cha Taaluma na Utafiti.
Rais Magufuli amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi
wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 March,
2018.
Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Mlingi Elisha Mkucha ambaye
atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Prof. Gabagambi alikuwa
Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine (SUA).
Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwakuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.
Mhe. Rais Magufuli
amemteua Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali
ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa
akikaimu nafasi hiyo.
No comments