Rais Mugabe Amtumbua Makamu Wa Rais
Emmerson Mnangagwa
Taarifa kutoka Harare zinasema kwamba, Makamu
wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amefutwa kazi.
Bw. Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75,
ameachishwa kazi kwa madai kuwa alionyesha tabia za kukosa uzalendo na uaminifu
hasa kwa Rais.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari wa Zimbabwe
Simon Kahaya Moyo.
Kufutwa kwake ni ishara kuwa mke wa rais Robert
Muabe, Bi Grace, atafuata nyayo za mumeme za kuwa rais wa Zimbabwe.
Siku ya Jumapili Bi Grace Mugabe alitoa wito wa
kutaka mumewe amfute kazi Mnangagwa.
Bwana Mnangagwa, ambaye ni mkuu wa zamani wa
idara ya ujasusi, amekuwa kwenye mstari wa mbele kumrithi Rais Mugabe.
Kufutwa kwake kunakuja baada ya Rais Robert
Mugabe, 93, kutishia kumuachisha kazi Bw Mnangagwa, hatua ambayo imezua uvumi
kuwa anataka mke wake kuchukua hatamu za kuliongoza taifa hilo.
Akihutubia mkutano wa wanachama wa makanisa ya
asili mji Harare siku ya Jumapili, Bi Mugabe alisema:
"Nyoka ni lazima apiwe kwenye kichwa.
Lazima tukabiliane na nyoka mwenyewe anayehusika na migawanyiko chamani.
Tunaelekea kwenye mkutano tukiwa chama kimoja."
Bw Mugabe alimtaka Mnangagwa na wafuasi wake
kumuonyesha uzalendo au afutwe kazi.
Chama cha Zanu-PF kinatarajiwa kuifanyia
mabadiliko katiba yake wakati wa mkutano na kuweka nafasi mbili za makamu wa
rais, nafasi moja ikiwa ni ya mwanamke.
Nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Bi Mugabe na
kuongeza uwezekano wa kumrithi mume wake.
Chanzo-BBC
No comments