Nyalandu Amtembelea Lowassa Ofisini Kwake
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini
(CCM), Lazaro Nyalandu amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati
Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Nyalandu aliyejiondoa CCM wiki iliyopita leo
Jumanne Novemba 7,2017 amemshukuru Lowassa kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa
kuna maisha nje ya CCM.
“Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema
asante kutufungulia mlango,” amesema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na
ofisi ya Lowassa.
Kwa upande wake, Lowassa aliyetoka CCM mwaka
2015 amemkaribisha Nyalandu upinzani akisema, “Nimefarijika kuja huku karibu
sana tushirikiane na kwa hakika 2020 tutavuka daraja.”
No comments