Naibu Waziri Dk.Ndungulile Azindua Cheti Cha Mfumo Wa Uhakiki Ubora Wa Huduma Katika Kiwango Cha Kimataifa Tfda
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine
Ndugulile akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki
Ubora wa Huduma cha Kiwango cha Kimataifa (ISO 9001:2015) leo Jijini Dar es
Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na
udhibiti wa ubora wa chakula na dawa katika ukanda wa Afrika Masharika
kutunikiwa cheti hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile na watendaji wa TFDA wakiwa wameshishika cheti cha
mfumo wa Uhakiki Bora katika Kiwango cha Kimataifa Cha ISO 9001-2015.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akitoa maelekezo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo wakatikati na Mwenyekiti wa
Bodi ya TFDA Dkt Ben Moses.
Meneja Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo
mbele ya Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile wakati akitembelea maabara katika
viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti
Sillo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia baadhi ya bidhaa zinazopelekwa TFDA kwa ajili ya
Uchunguzi.
Dar es salaam:
Naibu
Waziri Wa Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile ameitaka Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi TFDA kuendelea
kuboresha mifumo ya udhibiti wa uingizaji wa Dawa, Vipodozi na Chakula
nchini ili kulinda afya ya Watanzania.
Akizungumza mapema leo jijini dar es salaam mara baada ya kuzindua cheti
cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma katika kiwango cha kimataifa cha ISO
9001-2015 alisema mamlaka hiyo imekuwa ikitekeleza maujukumu yake kwa ufanisi
zaidi jambo katika kuhakikisha kuwa afya zinalindwa na kuwa na wanachi wenye afya
njema kuweza kufanya kazi kuliletea maendeleo taifa katika ujenzi ujenzi wa
uchumi wa viwanda.
“Dawa ni kitu nyeti sana, hatuwezi kuruhusu dawa feki kuingia nchini,
mnafanya kazi nzuri sana katika nyanja hii na muendelee na mpango huu ili
kudhibiti uingizaji wa vyakula visivyokidhi viwango na mahitaji ya watanzania,
” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa TFDA kwa kushirikiana na Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) wanatakiwa kuhakikisha wanazingatia miongozo ya
kupitisha vyakula na vipodozi kwenye mipaka ya nchi kwa kuzingatia ubora na
viwango vilivyoweka hili kudhibiti uingizaji mbovu wa vyakula visivyo na ubora.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Silo alisema ili
kuendelea kukidhi matakwa ya wateja na mahitaji yao wameamua kuendana na
kiwango cha kimataifa na kuwaita ISO kuja kuhakiki ambapo wamefanikiwa kukidhi
na kupata cheti.
“Shirika la Viwango la Kimataifa ISO limehakiki ubora wa huduma zetu
katika kukidhi mahitaji na matakwa ya watumiaji wa huduma zetu na kutupatia
cheti kinachoturuhusu kutoa huduma nchini” alisema Bw. Sillo.
Aidha Bw. Sillo aliongeza kuwa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi TFDA itaendelea kutekeleza majukumu yake bega
kwa bega na Serikali ya awamu ya tano ianyoongozwa na Rais Dkt. John pombe
Magufuli katika kusogeza mbele gurudumu la afya hapa nchini kupitia taasisi
ya hiyo.
No comments