Meya Chaulembo: Viongozi Jadilini Taarifa Kutoka Katika Kata Zenu Kutatua Kero Za Wananchi
Meya Wa manispaa ya Temeke Mhe. Abdallah Chaurembo
Na Sala Mlawas:
Wito umetolewa kwa viongozi Wa manispaa ya Temeke
jijini dar es salaam kushirikiana bega kwa bega kujadili taarifa zinazotokea
katika kata zao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Akizungumza na
waandishi Wa habari jijini Dar es salaam Meya Wa manispaa ya Temeke Mhe.
Abdallah Chaurembo alisema wanapaswa katika vikao vyao wazingatie asilimia 10
ya vijana na wanawake katika kuwapatia mikopo.
Aidha Mhe Chaurembo
ameongeza kuwa endapo watawapatia mikopo wanawake na vijana itasaidia kupunguza
baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi katika manispaa ya Temeke.
“Viongozi jadilini mijadala inayolenga kutatua changamoto zinazoikabili manispaa hiyo kwa weledi, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kukusanya mapato yatakayo kidhi mahitaji ya wananchi” Alisema Mhe Chaurembo.
Kwa upande wake
Afisa kutoka mamlaka ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU), Wilaya ya Temeke
Bi Estha mkokota Aliwataka viongozi kufwata sheria kanuni na taratibu za
utumishi wa umma zilizopo katika kutekeleza majukumu yao ili wananchi wapate
huduma kwa wakati uliopangwa.
Alisema kwa
kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono jitihada za serikali ya wamu ya tano
inayoongozwa na Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo Kwani miradi ya
maendeleo inayohusisha fedha za serikali inaletwa kwa lengo la kutatua kero za
wananchi .
No comments