Nape Awataka Watanzania Waache Ushamba
Mbunge wa Mtama, kwa tiketi ya (CCM) Nape Moses
Nnauye amefunguka na kuwataka watu kuacha ushamba kwani kusifu au kukosoa juu
ya jambo fulani ni kazi ambazo Mungu amewapa watu kuzifanya hivyo mtu baki
hupaswi kukerwa na kuhangaika na hayo.
Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa
Twitter na kusema mtu ambaye anachukizwa na watu ambao wana sifu juu ya jambo
fulani au kukosoa basi huyo mtu ni mshamba.
"Mungu kagawanya kazi, wengine kusifu,
wengine kukosoa, wengine yote pamoja! Kwanini unakerwa na kuhangaika na
mgawanyo wa kazi? !Acha ushamba" alisistiza Nape Nnauye
Aidha kiongozi huyo amezidi kusisitiza kuwa watu
wanapaswa kutimiza wajibu wao na kuacha kuhangaika na watu ambao wanasifia juu
ya mambo au kukosoa.
No comments